Waziri wa Michezo , Sanaa na
Utamaduni Mohamed Mchengerwa ameitaka Timu ya Wasichana ya Serengeti
chini ya Miaka 17 kuhakikisha wanarudi na kombe katika michuano
itakayoanza Oktoba nchini India.
Mchengerwa ameyasema hayo leo
wakati wa Kuaga Timu Serengeti Chini ya Miaka 17 katika hafla
iliyofanyika jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kwa udhamini wa wadau
wana imani ya kupata ushindi wa kurudi na kombe.
Amesema kuwa
Serikali imeweka mikakati ya kuimarisha timu ya Taifa kwa mpira wa miguu
kutokana na kuchoka kuwa kichwa cha mwenda wazimu.
Mchengerwa
amesema kuwa timu U-17 ya wasichana inakwenda kuweka kambi nchini
Uingereza ambapo kwa timu hiyo kwao ni kujifunza na kubadilisha
mazingira kwa kwa serikali ni kupata matokeo chanya.
Shirika la
bima la Taifa (NIC) limekabidhi bima ya Afya yenye thamani ya shilingi
Milioni 40 kwa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17
(Serengeti Girls) kwa ajili ya bima ya kuwalinda wakiwa majanga
watayopata wakiwa nje ya nchi na timu ya taifa ya Walemavu (Tembo
Warriors National Team) wakati wakijiandaa kushiriki michuano ya kombe
la Dunia.
Waziri wa Mchengerwa ameipongeza NIC kwa kuamua
kushiriki kwa namna moja katika kusaidia timu hiyo kwenda kufanya vizuri
katika michuano ya kombe la Dunia.
Aidha amewataka wachezaji
wakapambane na kuweza kufanya vizui kwenye michuano hiyo kwani uwepo wa
bima hiyo itaweza kuwasaidia pindi wanapopata changamoto katika michezo
waweze kusaidika kwa urahisi na kwa haraka.
Hata hivyo amewataka
wachezaji hao kutanguliza uzalendo wa nchi yao kwa kuhakikisha
wanapambana na kufanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano
Nae
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Elirehema
Doriye amesema kuwa kwa wale wachezaji watakaoumia kila wiki watakuwa
wanapewa laki moja kwa kipindi ambacho amekaa mpaka kufikia milioni 10,
hivyo amewataka wachezaji hao kupambana na wasiogope kuumia kwa timu
zote.
Amesema timu hizo ikifanya vizuri na kufika hatua ya robo
fainali, watazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 40, wakifika nusu
fainali watawazawadia shilingi milioni 80 na wakifika hatua ya fainali
watapatiwa milioni 100.
"Mnatakiwa mkapambana na kuhakikisha
mnaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, mkafanye vizuri na msigope
kuumia hata hivyo ikitokea mchezaji akapata kilema cha kudumu atalipwa
hivyo basi NIC ipo kwaajili yenu na tunawatakia kila la heri kwenye
michuano hiyo". Amesema Dk..Doriye.
Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa akizungumza katika hafla ya kuaga Timu ya Wasichana ya Serengeti chini ya miaka 17 inayokwenda kushirika Kombe la Dunia nchini India katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa akizungumza katika hafla ya kuaga Timu ya Wasichana ya Serengeti chini ya miaka 17 inayokwenda kushirika Kombe la Dunia nchini India katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni Dk.Hassan Abbas akitoa maelezo kuhusiana na Wizara ilivyoweka mikakati ya kuimarisha michezo katika hafla ya kuaga Timu ya Wasichana ya Serengeti chini ya miaka 17 inayokwenda kushirika Kombe la Dunia nchini India katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Dk.Elirehema Doriye akizungumza kuhusiana na Udhamini wa Timu za Taifa za Serengeti U-17 na Timu ya Walemavu zinazoshiriki Mashindano ya Dunia hivi karibuni wakati wa hafla ya kuiaga timu ya Serengeti U-17 iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa akipokea hundi ya Sh.Milioni 40 kwa ajili ya majanga ya timu za Serengeti U-17 na Timu ya Walemavu kwa ajili ya kusaidia majanga mbalimbali wakiwa nje ya nchi katika hafla ya kuaga Timu ya Wasichana ya Serengeti chini ya miaka 17 inayokwenda kushiriki Kombe la Dunia nchini India hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Timu ya Taifa ya Wasichana ya Serengeti U-17 wakiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Mohamed Mchengerwa akiambatana viongozi na watendaji wa Wizara hiyo.
Baadhi ya wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wasichana ya Serengeti U-17 wakisikiliza nondo za viongozi
No comments:
Post a Comment