Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge ametoa tahadhari kwa wananchi wa
Pwani na Dar es Salaam kuwa waangalifu wa matumizi ya maji kutokana na
hali ya upungufu.
Akizungumza
na waandishi wa wa habari Kunenge amesema mwaka jana kulikuwa na
changamoto ya upatikanaji wa maji hivyo mwaka huu hatutarajii kuwepo kwa
upungufu wa maji kwani maji ni uhai na wananchi hivyo anatoa tahathari
mapema ili kuondokana na uhaba wa maji kwa Mkoa wa Pwani na Dar es
Salaam.
"Ni
wajibu wetu kama viongozi tuliopewa dhamana kusimamia Rasilimali zetu
za maji zinalindwa vizuri na kutumika vizuri." Alisema Kunenge
Pia
amesema kuwa kulingana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na taarifa za
tahadhari za Mamlaka ya Hali ya Hewa inaonesha kipindi hiki hakutakuwa
na mvua za kutosha hivyo inabidi kusimamia vyanzo vya maji ili kuweza
kuondokana na upungufu wa maji kwenye Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam
"Tunapoona
kiwango cha upatikanaji wa maji kinaendelea kutokuwa himilivu kulingana
na mahitaji yetu ya kawaida kwa ajili ya kulinda uhai Dar Es Salaam
kuanza kutumia maji kwa uhangalifu kwa kuacha kutumia maji hovyo kwa
kuamini kuwa unaweza kulipa bili za maji." Alisema Kunenge
Pia
ameushukuru uongozi wa Mamlaka ya maji na usafi wa Mazingira (DAWASA)
pamoja na Bonde la Wami-Ruvu kwa kufuatilia kwa karibu hali ya maji hasa
kwenye mto Ruvu.
"Nafahamu
kuna baadhi ya Wananchi wameishapewa vibali vya kutumia maji kwa
shughuli za kilimo na najua mmeishawapa taarifa ya kutoendeleza mashamba
yao kwa sasa ili wasitumie maji kwenye shughuli ya kilimo kwa kipindi
hiki." Alisema Kunenge
Kunenge
amesema kuwa wale wote wenye vibali halali na bado wanaendelea kutumia
maji kwa shughuli za kilimo wasitumie mara moja mpaka watakapopewa
taarifa huku wakiangalia mwendendo mzima wa upatikanaji wa maji.
Amesisitiza
kuwa wale wote ambao hawataki kuzingatia Sheria hasa wanaohujumu
miundombinu ya maji, wizi, wanaotumia maji bila kufuata Sheria na
taratibu na wale wote wanaoleta mifugo kwenye vyanzo vya maji kuacha
mara moja.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu tahadhari zinazobidi kuchukuliwa ili kusiwepo
na changamoto ya upatikanaji wa maji kwa Mkoa wa Pwani na Dar es
Salaam. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi
wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Cyprian Luhemejana kulia ni Kaimu
Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy
Baadhi ya wakurugenzj wa DAWASA pamoja na mfanyakazi wa Ofisi ya mkuu wa Mkoa wa Pwani wakifuatilia mkutano wa mkuu wa Mkoa




No comments:
Post a Comment