Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
NAIBU
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewahakikishia wananchi wa
Mkuranga kwamba serikali itajenga mwaka huu madaraja matatu
yaliyoainishwa kwa ujenzi kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni tatu.
Waziri
Ulega ameuambia mkutano wa hadhara hapa jana kwamba serikali imetenga
fedha hiyo ili Jimbo la Mkuranga lifunguke kiuchumi. Bw Ulega ni mbunge
wa Mkuranga.
Amewambia
wananchi kwamba serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongwa na Rais
Samia Hassan imetoa fedha hiyo kutekeleza ahadi yake ya kurahisisha
usafiri na usafirishaji ili miradi ya maendeleo itekelezwe vizuri na
kipato cha wananchi kiongezeke.
“Lengo
la serikali ni kuliunganisha jimbo letu la Mkuranga na maeneo mengine
ili kuinua uchumi wa jimbo letu. Tukiweza kufanya biashara kwa urahisi
jimbo letu kufunguka kiuchumi,” alieleza Naibu Waziri Ulega na kufafanua
kwamba Mkuranga itafunguka kiuchumi “kwa kuwa mazao tunayozalisha
tutayafikisha sokoni kwa urahisi tofauti na hali ilivyo sasa kwani
wananchi wanakabiliwa na adha ya usafiri na usafirishaji.”
Aliyataja
madaraja yatakayojengwa kuwa ni daraja litakalounganisha Shungubweni na
Marogolo na Kongo Mulanzi. Daraja la Msolwa litakalounganisha Kisahani
naMalela na Nguja Kilamba mapaka Tipo. “Haya madaraji ni muhimku katika
kulifungua jimbo letu kiuchumi,” alisema Bw.Ulega
Alialeza
kuwa awali zilitengawa shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa
madaraja likini kutokana na umuhumu wa miundombinu katika jimbo la
Mkuranga Rais Hassan ameongeza fedha mpaka kufikia shilingi bilioni tatu
kwa ajili ya maendeleo ya wilaya nzima ya Mkuranga. “Huu ni ushahidi wa
dhamira ya serikali kumfikishia mwananchi maendeleo,” alisema.
Bw
Ulega alitoa rai kwa wajenzi wa madaraja hayo kuyajenga kwa wakati,
ufanisi na kutumia fedha kwa nidhamu ili ubora wa madaraja uendane na
thamani ya fedha iliyotolewa. “Tujitahidi kutekeleza ujenzi kwa wakati
na thamani ya fedha tuliyopewa ionekane. Tikiyatimiza haya itakuwa
rahisi kupata fedha nyingine kutoka serikalini kwa ajili ya maendeleo ya
jimbo letu,” alifanua.
Mkuranga
inazalisha mazao ya kilimo ya bishara, mboga na matunda na bidhaa za
uvuvi na misitu ambavyo vinatakiwa kufika sokoni kwa wakati ili kuongeza
kipato cha wananchi na kuinua uchumi wa Wilaya ya Mkuranga.
No comments:
Post a Comment