
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) inashirkiana na Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar (SMZ) katika kutekeleza program na miradi mbalimbali
ya hifadhi na usimamizi wa mazingira inayotekelezwa chini ya mikataba ya
kimataifa.
Hayo
yamesemwa na Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na
Mazingira) Mhe. Khamis Hamza Khamis wakati akijibu maswali bungeni
jijini Dodoma leo Septemba 13, 2022.
Katika
swali la msingi Mbunge wa Viti Maalumu Mhe. Maryam Azan Mwinyi alitaka
kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kuunda kikosi kazi kuratibu
Mikataba ya Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi kati ya Tanzania Bara
na Zanzibar.
Mhe.
Khamis alisema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi mwanachama wa
Mikataba mbalimbali ya kimataifa ya Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
ambayo inaratibiwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais.
Aliongeza
kuwa utaratibu unaotumika katika kuratibu masuala ya mikataba ya
Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi kwa pande zote mbili za Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
Hivyo
naibu waziri huyo alifafanua kuwa utaratibu huo ni wa kushirikiana
katika majadiliano, pamoja na kushiriki katika mikutano ya kimataifa na
utekelezaji wa mikataba hiyo.
Aidha,
alisema kuwa majadiliano yanayoshrikisha pande mbili za Muungano katika
masuala ya mazingira na mikataba yua kimataifa yapo kwa mujibu wa
sheria na kuwa mawaziri wa pande hizo mbili wanakutana na kujadiliana.
Kwa
upande mwingine alitaja miradi ya kimazingira inayotekelezwa kwa upande
wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar kuwa ni Mradi wa ujenzi wa kuta
za kupunguza kasi ya maji ya bahari Mtwara Mikindani na Wilaya ya
Kaskazini A, Zanzibar.
Pia
Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi kwa Kutumia Mifumo Ikolojia
Vijijini (EBARR) unaotekelezwa Wilaya ya Mvomero (Morogoro), Simanjiro
(Manyara), Kaskazini A (Unguja). Kishapu (Shinyanga) na Mpwapwa
(Dodoma).
Mradi
wa Kurejesha Ardhi iliyoharibika na kuongeza Usalama wa Chakula katika
maeneo kame Tanzania (LDFS) unatekelezwa katika Wilaya ya Nzega
(Tabora), Kondoa (Dodoma), Mkalama (Singida), Magu (Mwanza) na Micheweni
(Pemba).
No comments:
Post a Comment