Na.WAF, New York, Marekani
Tanzania
itapokea msaada wa Dola Milioni 15 (taribani shilingi Bilioni 34)
kutoka Kampuni ya Vodafone ili kuwezesha usafiri wa dharura kwa
wajawazito.
Ahadi hiyo imetolewa katika kikao cha pembezoni cha
Mkutano Mkuu wa 77 wa Wakuu wa Nchi (UNGA) unaoendelea Jijini New York,
Marekani.
Katika kikao hicho, chini ya Uenyekiti wa Mtendaji
Mkuu wa Shirika la misaada la Marekani (USAID), Bibi Samantha Power,
Mkuu wa Masuala ya Kimataifa wa kampuni ya Vodafone Bw. Joachim Reiter
aliwasilisha ahadi ya kampuni hiyo kutoa fedha hizo ili kutekeleza mradi
huo ikiwa ni hatua ya kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan za kukuza uchumi nchini.
Alieleza kuwa makampuni binafsi yana jukumu muhimu la kushirikiana na serikali kuleta maendeleo na kuchangia ustawi wa jamii.
Serikali ya Marekani kupitia USAID huzipatia pia kampuni binafsi fedha kuwezesha kufikia nchi zenye uhitaji mkubwa.
Akimwakilisha Rais Samia katika mkutano huo, Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango, aliishukuru Vodafone.
Dkt.
Mpango alieleza kuwa nchini Tanzania takribani wanawake 4,000 na watoto
65,000 hufariki kila mwaka huku kuchelewa kupata huduma za dharura
ikiwa ni pamoja na usafiri wa dharura kukichangia sehemu ya vifo hivyo .
Naye,
Waziri wa Afya Ummy mwalimu aliyeambatana na Makamu wa Rais katika
mkutano huo, alieleza furaha yake kwa Tanzania kupatiwa mradi huo.
Alisema
mradi huo utaisaidia Tanzania kufikia malengo iliyojiwekea katika
Mkakati wa Tano wa Afya na Mpango Mkakati wa Tatu wa Afya ya Uzazi, Mama
na Mtoto (one plan 3) ambayo moja ya vipaumbele ni kupunguza vifo vya
wajawazito na watoto na hivyo ni chachu ya kuiwezesha nchi kufikia
malengo endelevu ya kidunia.
No comments:
Post a Comment