DIWANI
wa Kata ya Loiborsoit Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Siria Baraka
Kiduya ameitaka Halmashauri ya Wilaya hiyo kutatua mgogoro wa ardhi
baina ya kata yake na kata ya Edonyongijape.
Kiduya
ameyasema hayo kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo cha kujadili changamoto na mafanikio ya kata zao.
Amesema
wananchi wa kata ya Loiborsoit wanasikitishwa ba kitendo cha baadhi ya
wananchi wa kata ya Edonyongijape kulima mazao yao kwenye eneo la kata
yao.
"Wataalam
wa ardhi wanapaswa kutuonyesha mahali mpaka ulipo ili wananchi wetu
wabaini na kufanya shughuli zao za maendeleo bila tatizo lolote,"
amesema Kiduya.
Diwani
wa Kata ya Edonyongijape, Jacob Kimeso ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti
wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, amesema baadhi ya wataalam wa
idara ya ardhi wamekuwa wakiwachangaya wananchi kwani wanakuja na ramani
tofauti.
"Leo
unawaambia wananchi mpaka wenu mwisho wake ni hapa kesho unawaambia
mwisho ni kule hawataelewa zaidi ya kuwachanganya," amesema Kimeso.
Kwa
upande wake Ofisa ardhi wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Baltazari
Sulle amesema mpaka unaotambulika hadi hivi sasa ni ule wa mwaka 1991
Wilaya ya Simanjiro ikiwa ipo Wilaya ya Kiteto.
Sulle
amesema Wizara ya Ardhi bado inatambua mpaka wa awali wa Loiborsoit na
Edonyongijape kwani huo mwingine wa mwaka 2012 uliofanywa na mradi wa
LAMP hautambuliki wizarani.
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Baraka Kanunga amesema wataalam
wa ardhi wanapaswa kuwashurikisha wananchi na viongozi husika ili
kuepuka migogoro.
Diwani
wa Kata ya Ruvu Remit Yohana Maitei Kadogoo amewataka viongozi
kukubaliana na suala la mipaka kwani jambo la kuhofia kupoteza wapiga
kura siyo lao ni Mungu anajua.

Diwani wa Kata ya Loiborsoit Siria Baraka Kiduya akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani.
No comments:
Post a Comment