Na Pamela Mollel,Arusha
Serikali
Mkoa Arusha imeanza mkakati maalumu wa kutenga maeneo ya kuhifadhi
wagonjwa wa ebola endapo watatokea kutokana na kuripotiwa ugonjwa huo
kuwepo nchi jirani
Akizungumza katika kikao cha afya ya msingi
kilichoshirikisha Viongozi na wadau wa afya jijini Arusha Mkuu wa Mkoa
Arusha John Mongella amewataka wataalamu wa afya kutoa elimu kwa
wananchi juu ya ugonjwa wa Ebola na namna ya kuchukua tahadhari
Mongella alisema kuwa wananchi wakipewa elimu ya kutosha itasaidia wao kuchukua tahadhari kabla ya hatari
"Hii elimu pelekeni vijijini wananchi huko hawana uelewa juu ya uwepo wa ugonjwa wa hatarii wa Ebola "alisema Mongella
Kwa
upande Mganga Mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Sylvia Mamkwe alisema kuwa
lengo la kikao hicho ni kujadili kwa kina namna ya kuchukua tahadhari
endapo ugonjwa huo utaingia nchi
Amesema kwa sasa hakuna mgonjwa
aliyeripotiwa kuwa na ugonjwa huo hatari na serikali inaendelea kuchukua
hatua namna ya kukabiliana nao
Aidha mamkwe alisema jumla ya watumishi 122 wa afya wameandaliwa kutoa elimu katika maeneo mbalimbali vijijini
"Kwa
sasa tunakabiliwa na changamoto ya vifaa ila serikali inapambana
kuhakikisha inapata vifaa vya kukabiliana na ugonjwa huo"alisema Mamkwe
Dalili za ebola ni kutoka kwa damu maeneo mbalimbali ya mwili kama vile masikioni,mdomono,puani Mganga mkuu wa mkoa wa Arusha Dkt Sylvia Mamkwe akizungumza na vyombo
Viongozi
na wadau wa sekta ya afya jiji la Arusha wakiwa katika kikao maalum cha
kujadili namna ya kuchukua tahadhari endapo ugonjwa huo utaingia nchini
Thursday, October 13, 2022
New
SERIKALI YATENGA MAENEO YA KUHIFADHI WAGONJWA WA EBOLA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment