Wakati
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akitimiza
Takribani Siku 560 za uwepo wake Madarakani, Rai imetolewa kwa Wananchi
kujitokeza Kushiriki kwenye Tamasha la Maombezi ili aweze kutimiza
majukumu yake kwa ajili ya Watanzania.
Mwito huo umetolewa Jijini
Dar es Salaam leo Oktoba 13, 2022 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama
Promotion inayoandaa matamasha mbalimbali ya injili nchini, Alex Msama
wakati akitambulisha Tamasha la Maombezi kwa ajili ya Rais Samia Suluhu
Hassan na Taifa kwa Ujumla.
Msama amesema Tamasha hilo ambalo
litahusisha Waimbaji mbalimbali wa nyimbo za Injili wa Ndani na Nje ya
Nchi, limelenga kuiweka Tanzania kwenye maombi pamoja na Rais Samia
Suluhu Hassan.
"Tunajua Rais wetu mama Samia Suluhu Hassan ni
Mchapakazi na amejitoa kwa ajili ya Kuwatumikia Watanzania, kwa hiyo
Dhamira ya Tamasha hili ni Kufanya Maombezi kwa ajili ya Kumuomba Mungu
aweze kumfanyia wepesi Rais wetu kwenye Utekelezaji wa majukumu yake ya
Kila Siku kwa ajili ya Watanzania" amesema Msama.
Ameongeza kuwa
Tamasha hilo la Maombezi limepangwa Kufanyika Jijini Mwanza November 11,
2022 ambapo litaendelea kwenye mikoa mingine hapa nchini.
Kwa
Upande wake Mratibu wa Tamasha hilo Emmanuel Mabisa amesema mpaka Sasa
Maandalizi mbalimbali yamekamilika kwa Kuzungumza na Wachungaji pamoja
na Maaskofu mbalimbali kushiriki Tamasha hilo la Maombezi kwa ajili ya
Taifa.
"Tayari Wachungaji na Maaskofu mbalimbali wamethibitisha
kushiriki kwenye Tamasha hilo kwa ajili ya Kupiga maombi kwa ajili ya
Rais Wetu na Taifa kwa Ujumla kwa maana yatakuwa ni maombi ya Kitaifa"
ameeleza Mabisa.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha mbalimbali ya injili
nchini, Alex Msama akizungumza na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
leo Oktoba 13,2022 jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha la kumuombea Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Taifa kwa ujumla
litakalofanyika jijini Mwanza tarehe 6.11.2022 jijini Mwanza
Pichani kulia ni mmoja wa Waratibu
wa Tamasha hilo Emmanuel Mabisa akieleza namna Maandalizi
yanavyokwenda mpaka sasa mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
leo jijini Dar es Salaam amesema mpaka Sasa Maandalizi mbalimbali
yamekamilika kwa Kuzungumza na Wachungaji pamoja na Maaskofu mbalimbali
kushiriki Tamasha hilo la Maombezi kwa ajili ya Taifa.
No comments:
Post a Comment