Na Catherine Sungura,WAF-Misenyi
WAZIRI
wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu ameagiza kupelekwa kwa vifaa tiba ikiwemo
mashine ya usingizi na upasuaji ndani ya wiki moja kwenye kituo cha afya
cha Kabyaile kilichopo kata ya Ishozi Wilayani Misenyi ambacho
kimebainishwa kama kituo maalumu cha matibabu kwa wagonjwa
watakaopatikana na ugonjwa wa Ebola.
Waziri
Ummy ametoa agizo hili wakati alipofanya ziara katika kituo hicho na
kuonga huku akijibu maswali kutoka kwa wakazi wa kata ya Ishozi
waliofika kwenye kituo cha afya cha Kabyaile.
Amesema
kwamba watatekeleza maelekezo yote yanayotolewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tamzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuahidi kwamba
watayasimamia maelekezo yote yanayotolewa.
"Serikali
ya awamu ya sita chini ya Rais Samia kwa upande wa huduma za afya
inajikita kwenye ubora wa huduma hivyo vifaa tiba tutaleta maana yake
atakapotokea mgonjwa wa Ebola na anatakiwa kufanyiwa upasuaji tutafanya
tutampe wapi." Alihoji Waziri Ummy.
Hata
hivyo Waziri Ummy allmemwagiza mwakilishi wa Katibu Mkuu kufuatilia oda
ya vifaa tiba hivyo kwenye Bohari ya Dawa (MSD) imeenda lini na kama
kweli wameoda vifaa hivyo walivyo vitaja.
Kwa
upande wa Bima ya Afya kwa wote (UHC), Waziri Ummy aliwahimiza wananchi
kukata bima ya afya ambayo itawaondolea gharama za matibabu na
malalamiko ya kuchangia huduma za tiba pindi wanapougua.
"Bima
ya afya kwa wote itatuondolea malalamiko haya ya kuchangia,hatutampiga
faini mtu yeyote bali tutawahamasisha kila mtanzania kuwa na bima ya
afya".
Aidha,
Waziri Ummy amewataka watumishi wa afya hususani viongozi kusema
ukweli kwamba dawa hazipo na hivyo kuwataka kuboresha huduma katika
vituo vyao ili kuweza kutatua changamoto zilizopo na kuimarisha
upatikanaji wa huduma za afya ikiwemo dawa na vifaa tiba.
Vilevile
Waziri Ummy hakuacha kutoa elimu kwa wakazi hao kuhusu tishio la
ugonjwa wa Ebola na kuwakumbusha wananchi hao kuendelea kuchukua
tahadhari zote za kinga ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa maji
tiririka na sabuni,kuepuka kugusa
damu,matapishi,kamasi,mate,machozi,mkojo,kinyesi na majimaji mengine
yanayotoka mwilini mwa mtu mwenye dalili za Ebola.
No comments:
Post a Comment