Na John Walter-Manyara
Wazazi
na walezi wanaowafanyia ukatili watoto wao kwa kigezo cha adhabu
wametakiwa kuacha tabia hiyo kwa kuwa wanawasababishia Usugu katika
maisha yao na kupelekea vifo na kukatisha ndoto zao.
Aidha
wameshauriwa kutenga muda wa kuzungumza na watoto wao kwa kuwafundisha
maadili mema huku wakiaswa pindi wanapotoa adhabu iwe ya kumfunza
kitabia na sio kumfanyia ukatili.
Kwenye jamii ya Kitanzania
maswala ya haki za mama na mtoto yamekuwa na changamoto kwani wanawake
na watoto wako kwenye hatari zaidi kuliko makundi mengine hivyo ni
muhimu elimu inayohusu sheria zinazolinda haki zao zifahamike na
kuzingatiwa.
Hayo yamesemwa na Wakili Winifrida Manyanga ambae ni
mkurugenzi wa Inherital right wakati akizungumza kwenye kipindi cha
TOBONGE kinachorushwa Smile Fm redio na kuongeza kuwa kutofahamu sheria
kunasababisha watu kushindwa changamoto ya kushindwa kutetea haki zao.
Kwa
upande wake mtaalam wa maswala ya saikolojia Anti Sadaka amesema wazazi
wanapotoa adhabu hawatoi kwa nia ya kuumiza bali wanatoa adhabu kwa nia
ya mtoto aangalie alichokifanya asije kurudia tena.
"Hivyo sifa ya kwanza ya mzazi au mlezi ni kuwa na ule uwezo wa kudhibiti hisia zake anapokuwa na hasira"
Serikali
ya Tanzania ikishirikiana na mashirika mbalimbali inazidi kutoa elimu
kwa jamii kila uchwao kuhakikisha vitendo vya Ukatili kwa wanawake na
watoto vinakomesha huku kukiwa na namba maalum ya kuripoti vitendo hivyo
kwa kupiga simu ya bure 116.
Mwaka 2020 kwenye maadhimisho ya
siku 16 za kupinga ukatili, Serikali ilizindua programu hiyo tumizi GBV
Taarifa jijini Dar es salaam nchini Tanzania wakati huu wa siku 16 za
kupinga ukatili wa kijinsia, tukio ambalo liliandaliwa kwa pamoja na
mashirika ya Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania na wadau wengine.
sheria
ya mtoto ya mwaka 2009 imeainisha haki mbalimbali za mtoto ambazo jamii
inapaswa kuzingatia, haki hizo ni pamoja na haki ya kutobaguliwa, haki
ya kuwa na jina na uraia, haki ya kutunzwa na kukua akiwa na wazazi
wake, haki ya maoni, haki ya kulindwa kutokana na mateso au adhabu
zilizopitiliza. Ukiukaji wa haki hizi za mtoto zinaweza kupelekea
aliyekiuka akitiwa hatiani, kulipa faini ya shilingi Milioni tano au
kifungo cha miezi sita au vyote kwa pamoja.
No comments:
Post a Comment