-MIAKA 7 YA BMH: MKURUGENZI AELIMISHA KUHUSU BIMA YA AFYA KWA WOTE
Hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma leo Oktoba 13, imetimiza miaka saba tangu ilipoanza kutoa huduma za Afya Oktoba 13, 2015.
Mkurugenzi
Mtendaji Dkt, Alphonce Chandika amewajengea uwelewa juu ya Msuada wa
Sheria ya Bima ya Afya kwa wote wananchi waliyofika kupata huduma,
ambapo mesema lengo la Mswada huo ni kuhakikisha, kila mwananchi
anakuwa na uhakika wa kupata matibabu bila hofu.
“Ndugu zangu
baadhi yenu mnakuja hapa mara kwa mara kupata huduma, mnafahamu ugonjwa
haubishi hodi, bila kuwa na BIMA kuna wenzetu hulazimika kuuza hata
viwanja au nyumba wagharamie matibabu” Alidokeza, Dkt. Chandika.
Aidha,
alifafanua kuwa mantiki ya Mswaada wa BIMA ya Afya kwa wote ni
kuhakikisha kuwa, watu wengi wanachangia gharama za matibabu kabla
hawajafikwa na maradhi ili kutunisha mfuko hatimae mtu akiugua asikutane
na changamoto yoyote ya kukosa huduma kwa kushindwa kulipia gharama za
matibabu.
“Msingi wa BIMA ya Afya kwa wote, ni suala la upendo
zaidi, na baba wa Taifa Mwalimu Nyerere tunaeadhimisha siku yake kesho
alitufundisha kupendana, hivyo tunapochangia wengi, wakaugua baadhi
tunakuwa tumewasaidia” Alifafanua Dkt. Chandika.
Vile vile,
alieleza kuwa mapendekezo ya Mswada huo ni kwa kaya moja kuchangia
Shilingi 340,000 na kunufaisha wanafamilia sita, huku mtu mmoja
akitakiwa kuchangia kiasi cha shilingi 84,000 ili kupata huduma za Afya
kwa mwaka mzima.
“Nasisitiza kuwa serikali haina lengo la
kumlazimisha mtu kuchangi, bali itaweka mazingira rafiki yatakayomsukuma
kila mmoja kuona umuhimu wa kuchangia, na kwa kutumia mifumo ya TASAF
na Ustawi wa jamii itawatambua wasiyojiweza na kuwatengenezea mfumo wa
kupata matibabu bila usumbufu” Alisema Dkt. Chandika.
Shamrashamra
za kutimiza miaka hiyo saba zimeanza saa mbili asubuhi ya leo kwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Dkt. Alphonce Chandika kushiriki
kutoa huduma za msingi kwa wagonjwa, aliwapokea, kuzungumza nao na
kuwasaidia waliyohitaji kutembea kwa msaada wa kiti maalumu
(Wheelchair).
Kisha aliwashukuru wananchi waliyofika Hospitalini
hapo kwa kutoa mchango wao wa maoni, ambayo hupokewa na kufanyiwa kazi
kwa wakati na ndiyo umekuwa msingi wa maboresho mbalimbali ya huduma
katika Hospitali hiyo kiasi cha kuifanya kutambuliwa kama kinara kwa
Utoaji wa huduma bora za Afya kwa Hospitali zote nchini.
Kwa
asubuhi ya leo, sherehe hizo ziliahanikizwa na ukataji wa keki maalumu
ya miaka saba ya huduma katika Hospitali hiyo, ambayo ilikatwa kwa
ushirikiano wa Mteja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.
Baadaye alielekea katika wodi ya watoto wachanga na kutoa zawadi mabalimbali kwa watoto hao kama sehemu ya kurejesha kwa jamii.
Na. Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano Hospitali ya Benjamin Mkapa.
Thursday, October 13, 2022
New
Hospitali ya Benjamin Mkapa yaadhimisha miaka 7
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment