JESHI la Zimamoto na Uokoaji limetekeleza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan la kumpokea Majaliwa Jackson Samweli ambaye aliyetoa msaada kwa waliopata ajali ya Ndege ya Precision Air iliyotokea katika ziwa Victoria.
Katika Taarifa ya Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kamishna Jenerali John Masunga iliyotolewa leo Novemba 7,2022 na Msemaji wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Makao Makuu Dodoma, SACF - Puyo Nzalayaimisi imesema kuwa Majaliwa
anatarajiwa kuanza mafunzo ya Zimamoto na Uokoaji pamoja na ya Uaskari
katika Chuo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kilichopo Chogo Wilaya ya
Handeni Mkoa wa Tanga.
Ikumbukwe
kuwa tarehe Novemba 06, 2022 ilitokea ajali ya kuanguka kwa Ndege ya
Precision Air katika Ziwa Victoria, ajali hii ilisababisha majeruhi na
vifo. Majaliwa alionesha ujasiri wa hali ya juu, kwa kuokoa wahanga 24
wa tukio hilo.
"Kamishna
Jenerali anatoa shukrani za dhati kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama,
Taasisi za Umma na Binafsi, pamoja na Wananchi wa Mkoa wa Kagera kwa
ushirikiano mkubwa waliotoa katika zoezi la uokoaji katika ajali hiyo."
Pia
Kamishna Jenerali anatoa pole kwa Wafiwa wote na kuwaombea faraja
katika kipindi hiki kigumu wanachopitia, anawatakia majeruhi wote afya
njema.
Anawasihi
Wananchi kuendelea kushirikiana na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika
kuokoa Maisha ya watu na mali dhidi ya majanga mbalimbali.
No comments:
Post a Comment