WATU
Saba kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto, sita wa kada ya afya na
mmoja mwalimu, wamefariki dunia na wengine saba kujeruhiwa katika ajali
maeneo ya pori namba moja Wilayani Kiteto Mkoani Manyara.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kiteto, marehemu wawili ni mtu na mke wake, na
walikuwa na mtoto wao wa miezi tisa ambaye amenusurika.
Akithibitisha
ajali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Batenga amesema majeruhi
watano wamepelekwa Hospitali ya Benjamin Mkapa jijini Dodoma kwa ajili
ya matibabu zaidi na wawili wamebaki katika Hospitali ya Wilaya ya
Kiteto.
Amesema
ajali hiyo ilihusisha Gari la wagonjwa wa kituo cha afya Sunya
likitokea Kibaya kupeleka Mgonjwa, ambapo baada ya kumshusha Mgonjwa
njiani likagongana uso kwa uso na gari aina ya Prado ambayo ilikuwa
inatokea Kilindi kuelekea Kibaya.
No comments:
Post a Comment