Na Farida Mangube,Morogoro.
Ongezeko
na kukithili kwa matukio ya ukatili wa kijinsia nchini hasa kwa
wanawake na watoto kumechangia migogoro ya kifamilia, talaka na
kukosekana kwa malezi ya dhati kutoka kwa wazazi na walezi na kufanya
watoto kuishi mazingira hatarishi na mwingine kwenye vituo vya kulelea
watoto.
Carolyn Kezilahabi anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 14
mzaliwa wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, kwasasa anaishi kituo cha
Raya Orphanage Centre kilichopo Wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro, baada
ya kuchoshwa na manyanyaso na vipigo vya kila uchwao kutoka kwa
Shangazi yake.
Anasema miaka mitano iliyopita shangazi yake
alifika kijijini kwao na kumchukua kuja kuishi nae Dakawa Wilayani
Mvomero baada ya Bibi yake kufariki, shangazi huyo alimuahidi
kumuendeleza kimasomo, lakini walipofika Dakawa imekuwa tofauti.
Anasema
baada ya kufika Dakawa shangazi yake alianza kumnyanyasa na kumtesa kwa
kumpatia kikombe kimoja cha chai na chapati moja kama chakula cha siku
nzima.
“Shangazi yangu alikuwa nafanya biashara ya kupika chai
siku moja nilikuwa namimina chai kwa bahati mbaya nikadondosha chupa ya
chai na ikavunjika nikamwambia shangazi chupa imevunjika lakini
hakunielewa akaanza kunipiga na flampeni kichwani, na baadae kuchukua
panga, aliponyanyua panga kutaka kunipiga kichwani nikaweka mkono na
akanikata kwenye kidole.”alisema Carolyn
Aidha anasema baada ya
kipigo hicho alikimbia na kwenda kumueleza Mwalimu wake shule ya msingi
dakawa alipokuwa anasoma ambaye alimpeleka kwa Mwenyekiti wa Serikali za
Mitaa na kuweza kupata hifadhi kwa muda na ndipo safari yake ya kuanza
kuishi kwenye kituo cha kulelea watoto cha Raya Orphanage Centre.
Mtoto
huyo kwa sasa kilio chake kikubwa anatamani kukutana na kuwaona wazazi
wake ambao hajawaona wala kuwasikia hata kwa simu kwa zaidi ya miaka
mitano na kwamba sababu aliondoka Ukelewe akiwa katika umri mdogo hivyo
anashindwa kukumbuka amezaliwa kijiji gani.
Kilio cha Carolyn
ambaye amehitimu darasa la saba na anasubiri matokeo kwa sasa,kimekuja
baada viongozi wa Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa Morogoro
wakiongozwa na Kamishna wa forodha na ushuru wa bidhaa wa TRA makao
makuu Said Kiondo kutembelea kituo cha Raya wakati wa maadhimisho ya
wiki ya mlipa kodi.
Akizungumza na waandishi wa habari jana
Kamishna huyo Kiondo alisema TRA imeona ni vyema kurudisha faida kwa
jamii ambayo imekuwa mstari wa mbele kwenye ulipaji wa kodi.
Aidha
aliwataka watanzania kuendelea na utamaduni wa kudai lisiti halali za
bidhaa wanazonunua ili kustawisha uchumi wa nchi kwani wanabaadhi ya
wafanyabishara wamekuwa tabia ya kutoa risiti tofauti na kiasi
kilicholipwa na mteja.
Pia amewataka wafanyabiashara kuwasilisha
litani zao ndani ya muda uliopangwa kisheria kwani kwa kuchelewesha
kupeleka litani ndani kunapelekea usumbufu pamoja na kupigwa faini jambo
ambalo linamfanya mfanyabiashara kuongeza gharama kwenye biashara yake.
Kiondo
aliwataka Wananchi kulipa kodi kwa wakati kwani Tra kodi zake
zimepangwa kwa wakati na kuna kodi za siku, mwezi, robo ya mwaka na
mwaka moja hivyo akawasisitiza wananchi kulipa kodi hizo kwa wakati
kunaisaidia TRA kufanya kazi zake kwa ufanisi.
Kwa upande wake
mkurugenzi wa Kituo cha kulelea watoto yatima cha Raya Orphanage Raya
Subaha aliishukuru TRA Mkoa wa Morogoro kwa kuwatembelea na kuwafariji
watoto waishio katika kituo hicho na kwamba kwa sasa analea watoto 70.
Alisema
hicho kituo kimekuwa kikiwajengea watoto uwezo wa kujitambu kwa
kuwafundisha elimu ya dini pamoja na ile ya dunia na watoto wanakabiliwa
na changamoto ya kutembea umbali mrefu kufika shuleni huku kipindi cha
mvua kutokana na mito kujaa maji watoto ushindwa kuhudhuria masomo..
TRA
Mkoa wa Morogoro katika kuadhimisha wiki ya mlipa kodi wamefanya
shughuli mbalimbali ikiwemo kutoa elimu kwa walipa kodi pamoja na
kurejesha faida ya sehemu ya mapato yake katika jamii, kwa kutembelea
vituo vya kulea watoto na kutoa mahitaji mbalimbali ambapo wametembelea
kituo cha Mgolole pamoja na Raya vyote vya kulelea watoto yatima na
waliotelekezwa na wazazi wao ambapo waliwapatia zawadi mbalimbali.
Tuesday, November 22, 2022
New
TRA Morogoro yamuibua mtoto anayewatafuta wazazi wake hajawasiliana nao kwa zaidi ya miaka mitano.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment