Na Oscar Assenga,TANGA.
MAMLAKA
ya Mapato Tanzania Mkoani Tanga (TRA) leo wamekutana na kuzungumza na
walipa kodi Mkoani Tanga katika halfa iliyokwenda sambamba na
kuwapongeza kwa ulipaji kodi wao wa mwaka wa Fedha 2021/2022 ambao
uliiwezesha kuvuka lengo na kuibuka kidedea katika mikoa yota nchini.
Halfa
hiyo ilikwenda sambamba na kuwatembelea wateja wakubwa mkoani Tanga
ikiwemo wafanyabiashara katika eneo la barabara ya 14 Jijini Tanga na
Kiwanda cha PPTL ambako walizungumza nao.
Akizungumza
wakati wa halfa hiyo Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga Specioza Owure alisema
kwamba mamlaka hiyo kwa mwaka wa fedha 2022/2023 inakusudia kukusanya
kodi kiasi cha shilingi Billioni 232.69 ikiwa ni malengo ya serikali
sawa na ongezeko la asilimia 37 ya mwaka wa fedha uliopita.
Alisema
kutokana na uwepo wa Kutokana na ongezeko hilo alitumia fursa hiyo
kuwataka wafanyabiashara mkoa humo kuendelea kushirikiana kikamilifu na
mamlaka ya mapato katika kuhakikisha wanalipa kodi kwa wakati na kwa
hiari ili kuweza kufikia malengo yaliyowekwa ya kuendelea kung’ara
katika ukusanyaji wa kodi hapa nchini
Meneja
huyo alisema mamlaka hiyo kuibuka kidedea ni kutokana na walipa kodi wa
mkoa wa Tanga kulipa kodi na hivyo kuwawezesha kufanya vizuri katika
kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 .
Alisema
kwa mkoa wa Tanga walikuwa wamepangiwa lengo la kukusanya billion
169.68 lakini wao wameweza kukusanya billioni 207.52 ikiwa ni sawa na
asilimia 121.6% hivyo waliwashukuru kwa kuwawezesha kufikia lengo hilo.
Meneja
huyo alisema pia katika mwaka wa fedha 2022/2023 lengo lao la
ukusanyaji limeongezeka na kufikia bilion 63 ambayo ni sawa la ongezeko
la asilimia 37% ya lengo la mwaka huu ni bilion 232.69 kwa hiyo wana
kazi kubwa ya kufanya.
Alisema
kwa sababu mwaka uliopita waliweza hatua ambayo imepelekea mwaka huu
wameongezewa lakini katika hayo yote hatukuweza pekee yetu bali ni
ushirikiano wenu wadau na hivyo kuweza kulipa kodi kwa hiari
Hata
hivyo Meneja huyo aliwataka wafanyabiashara katika mkoa huo kuhakikisha
wanaendelea kulipa kodi pamoja na kutekeleza maagizo ya serikali ya
kulipa kodi kupitia mfumo wa kielektroniki.
“Lakini
pia niwatake kutoa taarifa kwa mamlaka ya mapato pale panapotokea
changamoto yoyote ikiwemo ya kusitisha biashara au kuhama”alisema
Awali
akizungumza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kanda ya Kaskazini
Selestini Kiria aliipongeza mamalaka hiyo kwa mafanikio waliyoyapata
kwa mwaka wa fedha uliopita.
Sambamba na hilo pia amewaomba kuendelea kuboresha huduma zao ili kuzidi kuwavutia wateja kuweza kulipa kodi kwa wakati.
Akizungumza
wakati alipotembelewa kwenye duka lake Mfanyabiashara Wilbard Mallya
aliipongeza mamlaka hiyo kwa huku akiiomba Serikali kuwaangalia
wafanyabiashara kwenye suala la kodi pamoja na kurahisisha utoaji wa
huduma. |
No comments:
Post a Comment