Baadhi
ya wakulima waliofika ofisi kwa m
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Halima Dendego ,
kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kwa kuboresha sekta ya Kilimo
Baadhi
ya wakulima waliofika ofisi kwa mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego
kwa ajili ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha sekta ya Kilimo.
Na Fredy Mgunda, Iringa.
WAKULIMA
mkoa wa Iringa wamefanya matembezi ya kumpongeza Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kuwapunguzia bei ya
mbolea.
Wakizungumza
Mbele ya Mkuu wa mkoa wa Iringa,wakulima hao wamesema kuwa walikuwa
wakinunua mbolea kwa shilingi 150,000 lakini sasa wananunua kwa
shilingi 60,000 hadi 70000
“Tunampongeza
na kumshukuru sana rais samia kwa kutuona sisi wakulima kwa sababu
mwanzo tulikuwa tukinunua mbolea kwa laki moja elfu thelathini lakini
saizi tunapata kwa elfu 60000 hadi sabini ni hatua nzuri tunampongeza
mama na sasa tunaamini kila mwananchi wetu atalima"walisema
Akisoma
risala Mbele ya Mkuu wa mkoa wa Iringa Abeid Kiponza alisema kuwa wana
kila sababu ya kumpongeza Rais Samia kutokana na kupunguza gharama za
pembejeo za kilimo hususani upande wa mbolea
“sisi
wakulima wa mkoa wa Iringa tumefanya matembezi maalumu ya kumshukuru na
kumpongeza mheshimiwa rais kutokana na upendo wake kwetu kutokana na
mambop makubwa anayoendelea kutufanyia kwenye kilimo tanzania nzima
inajua wakulima wa nyanda za juu kusini tumekuwa tukizalisha
viazi,mahindi,ngano,alizeti na mazao mengine ya chakula na hatuwezi
zalisha mazo vizuri bila kuungwa mkono na serikali na tumwambie
usiwasikilize wanasiasa ambao wamekuwa kama wasemaji wetu wakati sio
wasemaji wetu usiwasikilize"alisema
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Halima Dendego amesema kuwa
Serikali ya awamu ya sita imeamua kutatua matatizo ya msingi kwa
kuwekeza kwenye kilimo na miradi umwagiliaji.
“Sisi
wote ni mashuhuda mheshimiwa rasi ameweza kutoa pikip[iki kwa maafisa
ugani wote na wanatakiwa wahikikishe wanafika kama kuna maswali muulize
wawahudumie nyinyi na zimetoka billion 55 mradi wa pawaga umwagiliaji
kwa hiyo tunaposema mama ameupiga mwingi na ametuletea ruzuku ambayo
ndio tunategemea sisi wakulima"
Hata
hivyo lengo la serikali ya Rais Samia Suluhu awamu ya sita ni
kuhakikisha inaboresha sekta ya kilimo na maslahi ya wakulima kwa
ujumla.
No comments:
Post a Comment