Kamishna
wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela (kushoto) akishikana mkono na
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila
wakati wa kukabidhi Matanki ya Maji kwa ajili ya Hospitali hiyo.
Na Kadama Malunde
Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) imekabidhi matanki mawili ya kuhifadhia maji
yenye ujazo wa lita 20,000 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Shinyanga iliyopo Mwawaza katika Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu
ya maadhimisho ya Wiki ya Shukrani kwa Mlipa Kodi “Asante kwa kulipa kodi kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya taifa;Kazi Iendelee”.
Matanki
hayo yamekabidhiwa leo Alhamisi Novemba 24,2022 na Kamishna wa Kodi za
Ndani TRA, Herbert Kabyemela kwa Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa
Mkoa wa Shinyanga Dkt. John Luzila katika hospitali hiyo.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi matanki hayo mawili yenye ujazo wa lita 10,000 kila
moja, Kamishna wa Kodi za Ndani TRA, Herbert Kabyemela amesema TRA
imetoa matanki hayo ikiwa ni sehemu ya shukrani kwa walipa kodi ili
kupunguza changamoto ya vifaa vya kutunzia maji katika hospitali mpya ya
Rufaa Mkoa wa Shinyanga.
“Sisi
TRA tupo katika wiki ya shukrani kwa mlipa kodi iliyoanza Novemba 23
hadi Novemba 25,2022. Tumeleta matanki haya ili kupunguza changamoto ya
vifaa vya kutunzia maji kwenye hospitali hii ya Rufaa mkoa wa
Shinyanga”,amesema Kabyemela.
Akipokea
matanki hayo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga
Dkt. John Luzila ameishukuru TRA kwa kuikumbuka hospitali hiyo mpya na
kuipatia matanki ya kuhifadhia maji akibainisha kuwa hospitali hiyo
inahitaji maji kila wakati.
“TRA
mmefanya jambo jema kuleta matanki ya kuhifadhia maji, hili ni jambo
muhimu sana kwa sababu tunahitaji maji kila wakati kwa ajili ya huduma
mbalimbali katika hospitali hii mpya ambayo imeanza kufanya kazi hivi
karibuni hapa Mwawaza”,amesema Dkt. Luzila.
No comments:
Post a Comment