


Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi za Udhibiti wa huduma za Mafuta na Umeme kwa nchi
sita za Afrika Mashariki (EREA) Dkt. Geoffrey Mabea akizungumza na wadau
wa mafuta na gesi wakati wa mafunzo kwa wataalamu wa mafuta na gesi 230
kutoka nchi 27 Afrika kutambua namna ya kuandaa mikataba inayohusu
sekta hiyo ili kujiinua na kuchangia pato la Taifa.
Kushoto ni Dkt. Shirley Baldwin Mushi akipokea cheti kutoka kwa Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Ruth Mtoi Simba cha kutambua mafunzo aliyatoa kwa wadau wa Mafuta na gesi yaliyofanyika jijini Arusha.

Baadhi
ya Wadau wa Mafuta na Gesi wakiwa katika picha ya pamoja mara baada
kumalizika kwa mafunzo ya Mafuta na Gesi yaliyofanyika jijini Arusha.
Na Karama Kenyunko, Michuzi Blog
TAASISI
za Udhibiti wa huduma za Mafuta na Umeme kwa nchi sita za Afrika
Mashariki (EREA) iliyo chini ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC),
imesema mpaka sasa imetoa mafunzo kwa wataalamu wa mafuta na gesi 230
kutoka nchi 27 Afrika.
Imesema
mafunzo hayo yanalenga kuwafanya wataalamu watambue namna ya kuandaa
mikataba inayohusu mafuta na gesi na namna watakavyoshiriki kuinua sekta
ya mafuta na gesi na kuchangia pato la taifa.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa EREA, Dkt Geoffrey Mabea wakati
akizungumzia mafunzo wanayoyatoa kwa wadau wa mafuta na gesi, mafunzo
hayo yamefanyika jijini Arusha.
"Mafunzo
haya yamekuwa yakitolewa katika nchi mbalimbali lakini sisi tuliona
tuyafanyie hapa kwetu kwa kuwatumia watalaam wa ndani Dkt. Aloys Rugazia
na Dkt. Shirley Mushi ambapo tumeweza kuwakutanisha wataalamu wa nchi
za Tanzania na Kenya," amesema Dkt. Mabea.
Ameongeza
kuwa huu ni mwaka wa pili wanatoa mafunzo ya uelewa kuhusu sekta hiyo
na mpaka sasa wataalamu 230 wamenufaika na mafunzo wanayoyatoa kupitia
mtandao na chuoni.
Hata
hivyo, amesema katika mafunzo yaliyofanyika Novemba 14-18, 2022
wataalamu hao walijadiliana kwa kina kuhusu uchakataji wa mafuta ghafi
na gesi chini ya wakufunzi toka hapa hapa Tanzania, Dkt. Aloys Rugazia
na Dkt. Shirley Mushi na kushauri haja ya kuwepo kwa mitambo ya
Kuchakata Mafuta (Refinery) katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) ili nchi zipate manufaa yakuchakata Mafuta nyumbani badala
yakuagiza Mafuta ambayo yamechakatwa tayari.
Dkt.
Mabea ameeleza kuwa biashara ya mafuta imekuwa changamoto kubwa
kutokana na gharama zake hivyo wangekuwa na mitambo ya kuchakata mafuta
ghafi ingesaidia nchi za Afrika Mashariki kufanya biashara wenyewe na
hivyo kupunguza utegemezi na kudhibiti bei za Mafuta na mbolea
zitokanazo na Mafuta ghafi.
Ameongeza
kuwa taasisi hiyo ina jukumu la kuwaleta pamoja wadhibiti kwa lengo la
kupandisha miundo mbinu ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC) kusaidia nchi hizo kuwa na misingi bora ya udhibiti na kutekeleza
wajibu wao kwa kuwa na wataalamu wengi.
Amesema
wameanzisha Chuo kinachotoa mafunzo kwa wadhibiti kilichopo Arusha,
ambacho kinatoa mafunzo kuhusu nishati za mafuta na gesi na lengo ni
kuwaelimisha namna ya kuchimba na kuchakata gesi kwa matumizi.
No comments:
Post a Comment