NA
MAGRETHY KATENGU
CHAMA cha
ACT Wazalendo Chafafanua mambo matano ambayo Serikali inapaswa
kuyachukulia hatua ili kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mafuta ya
Petroli na Diseli nchini pia kupanda bei.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Waziri Kivuli wa Sekta ya
Nishati wa Chama hicho Isihaka Mchinjita amesema hivi karibuni mafuta hayo
yamepanda bei hivyo wameona hawawezi kukaa kimya wakaona watoe ushauri
serikali hatua zinazopaswa kuchukua ni ikiwemo , Serikali kuweka
msisitizo wa kupunguza matumizi ya mafuta ya Petroli na Diseli kwa kutumia
nishati mbadala ya Gesi asilia kuanzia kwenye magari ya serikali na mabasi
yaendayo mkoani.
"Inawezekana
kwa kuchukua hatua kadhaa za haraka ikiwemo magari yote ya Serikali kuanza
kutumia Gesi asilia (CNG) na bohari zote za Serikali (GPSA) zifungwe mitambo ya
kujazia gesi asilia (CNG) Vilevile, mabasi ya mwendokasi nayo yabadilishwe
mfumo na yaanze kutumia gesi asilia ,magari ya abiria ya mikoani (mabasi) yote
yafungwe mfumo wa kutumia mitungi ya Gesi asilia (CNG), ili kupunguza kutumia
fedha nyingi za kuagiza bidhaa za mafuta,” amesema Mchinjita.
Mchinjita
amefafanua kuwa hivi karibuni wanaoagiza mafuta nje ya nchi wanakumbana uhaba
wa dola kwani ndiyo fedha inayotumika kuagizia mafuta hivyo ni vyema
Serikali ianze kupunguza matumizi ya dola za Kimarekani kwa Benki Kuu kuruhusu
wanunuzi wa mafuta kulipia kwa shilingi kisha benki hiyo ndio iwalipe wanunuzi
wa nje kwa dola za Kimarekani ili kuwarahisishia wafanyabiashara ya mafuta
wasihangaike kutafuta dola.
Amesema
Tatu, hatua nyingine, ni kuhakikisha Serikali inadhibiti mahitaji ya dola kwa
kuhakikisha matumizi yote ya ndani yanafanywa kwa shilingi ya Tanzania nne,
kuongeza mauzo ya bidhaa za kilimo nje ikiwemo kuongeza thamani ya mazao
Awali
akizungumzia kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta ya petroli na diseli, amesema
katika uchambuzi wa Chama hicho walioufanya Agosti 2, 2023 ulijikita
zaidi katika kuangalia tatizo la kupanda kwa bei za mafuta na sababu
zilizopelekea kupaa huko na walitoa mapendekezo yao ili kushusha bei hizo
kwani hivi karibuni wamekuwa wakifuatilia kwa karibu zaidi juu ya
hali ya upatikanaji wa mafuta nchini na kwa mujibu wa utafiti wao wamebaini
kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa mafuta katika hifadhi ya mafuta
bandarini (Dar es Salaam).
Amebainisha
kwamba changamoto ya upatikanaji wa mafuta imepelekea waagizaji wa mafuta
hususani kwa waagizaji wadogo kuchelewa kupata mzigo kutoka bohari za bandari
ya Dar es Salaam kwani awali iliwachukua siku 1 tu sasa inachukua siku 3 hadi 4
kupata mafuta na kupakia katika Bohari za Dar es salaam jambo linalopelekea
uhaba katika maeneo mengi.
“Hali
katika bandari ya Mtwara imekuwa mbaya kwa mafuta ya petroli ambapo
hayapatikani kabisa, jambo linaloplekea wauzaji wote waliokuwa wanachukua
mafuta katika bandari ya Mtwara kulazimika kufuata Dar es Salaam,” ameeleza
Mchinjita.
Ingawa
wanafahamu uwezo wa nchi kuhifadhi mafuta ni wa mwezi mmoja, lakini tulikuwa
tunaagiza mafuta kwa kutangulia miezi miwili hivyo kwa sasa mafuta yanayotumika
ni yale yaliyoagizwa mwezi huu wa nane.
Kwamba
sababu kubwa inayopelekea kuwepo kwa tishio la uhaba wa mafuta nchini ni
kupungua kwa uwezo wa kuagiza mafuta kwa waagizaji wetu kutokana uhaba wa dola
pia kupanda juu pia tangu mwezi Machi kutokana na uhaba wa dola waagizaji
wamekuwa wakipunguza kiasi wanachoagiza.
Amesema
hii ni kutokana na uhaba wa dola za marekani na kushuka kwa thamani ya shilingi
ya Tanzania kwa dola, jambo linalopelekea waagizaji kupoteza kiasi kikubwa cha
fedha katika kubadilisha shilingi kwenda dola za marekani.
Amefafanua
kuwa katika hali hii Serikali haipaswi kusubiria miujiza kukabiliana na
changamoto hizi au kusubiri kutokea kwa athari kubwa zaidi ndio ichukue hatua
za kunusuru ni hatari ya Serikali kutochukua hatua za haraka ni kupelekea
kupandisha bei zaidi na kuongeza kiwango cha uhaba zaidi nchini.
Amesisitiza
kuwa tatizo la mafuta upatikanaji na gharama zake linahitaji hatua za makusudi
za Serikali.
Kwamba
ni muhimu kwa Serikali kuuza nje bidhaa zinazotokana na kilimo badala ya kuuza
malighaf pia kuweka vivutio katika sekta ya utalii kwa kuongeza matangazo na
kuboresha miundombinu ya Utalii ili kuongeza idadi ya watalii maradufu ya idadi
ya sasa.
"Tukifika
watalii Milioni 5 kwa mwaka, nchi yetu itapata fedha za kigeni mara tatu ya
tunazopata sasa na kuongeza ajira nyingi kwa watanzania," ameeleza
No comments:
Post a Comment