MKANDARASI wa Kampuni ya Help Desk, akiendelea na mchakato wa ufungaji wa tenki la chuma la kukusanyia maji lenye ukubwa wa lita laki tano katika eneo la Nzuguni jijini Dodoma.
Kupitia mradi wa maji wa Nzuguni zaidi ya lita za maji milioni
7.6 zitazalishwa kwa siku, hivyo kuongeza asilimia 11 za upatikanaji maji
katika Jiji la Dodoma na kuwanufaisha zaidi ya wakazi 75,968 kutoka maeneo ya
Nzuguni, Swaswa, Ilazo na Kisasa.
Mradi huo unagharimu kiasi cha shilingi bilioni 4.8 hadi
kukamilika kwake.
No comments:
Post a Comment