Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi akimkabidhi benders kiongozi wa vijana wanaokwenda kutembea kwa miguu katika mikoa 16 nchini kuunga mkono kazi za Rais Samia Suluhu Hassan na kuhimiza vijana kuchapa kazi, Abiudi Maugo, bendera ya taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mobhare Matinyi (katikati) akiwa na vijana wanaokwenda kutembea kwa miguu katika mikoa 16 nchini. Kulia kwa DC ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke na kushoto kwake ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Mtinika.
NA KHADIJA KALILI
MKUU wa Wilaya ya Temeke, Mobhare
Matinyi, amewaagiza vijana saba wazalendo ambao wameondoka Dar es Salaam
leo asubuhi kuanza matembezi ya mikoa 16 ambapo watazitangaza kazi zinazofanywa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
DC Matinyi amewakabidhi bendera ya taifa kwenye hafla
fupi iliyofanyika ofisini kwake asubuhi ya Agosti 15
2023 , amezitaja baadhi ya kazi zilizofanywa wilayani Temeke mwaka 2022/23
na thamani ya fedha zilizotolewa na Rais Samia kuwa ni pamoja na miradi ya afya
sh. bilioni6.1, elimu ya msingi sh. bilioni 7.6, elimu ya sekondari sh. bilioni
10, maji sh. bilioni 15.5, umeme sh. bilioni 61.6 na barabara sh. bilioni 43.7.
Amesema kwa ujumla Wilaya ya Temeke imepatiwa na Rais Samia zaidi sh.
bilioni 152 katika kipindi hicho kutokana na wingi wa wakaazi wake ambao
wanafikia milioni 1.35 na nia yake ya kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Aidha amewaaambia vijana hao kuwa katika kilomita 3,624
wanazotarajia kutembea kwa miguu watakutana na ushahidi lukuki wa kazi za
Rais Dkt. Samia.
Vijana hao saba wanaoongozwa na Abihudi Maugo wanatarajiwa kuhitimisha
matembezi yao Mkoani Manyara wakati wa sherehe za kuuzima mwenge hapo Oktoba
14, 2023.
Vijana wengine ni Sophia Kooni, Beatrice Masanja, Shabani Juma, Jesca
Giribert, Flora Ernest na Paul Mkinga.
No comments:
Post a Comment