BENKI ya NMB, kwa kushirikiana na Vodacom na Google, wamezindua kampeni ya ‘Miliki Simu, Lipa Mdogo Mdogo’, inayowezesha watanzania wa kipato cha chini na kati kumiliki simu janja (smartphone).
Katika kufanikisha hilo, Benki ya NMB imeingia makubaliano na kampuni ya
Vodacom ili kurahisisha upatikanaji wa mikopo ya simu janja hizo.
Katika kuwezesha urahisi wa malipo :
✅ Mteja ataweza kulipa kianzio cha
Tsh 20,000 kisha kulipa kuanzia Tsh 900 tu kwa siku.
✅ Mteja anaweza kuchagua pia kufanya
malipo kwa wiki au mwezi.
✅ Mteja anaweza kujiunga na huduma
hii kupitia menu ya M-Pesa, kisha kufika kwenye duka lolote la Vodacom kuchukua
simu yake.
✅ Kwa mwaka huu zitatolewa simu
milioni moja kwa wateja ambao watakidhi vigezo vya kukopeshwa.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo jijini Dar es
Salaam jana, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert
Mponzi alisema:
“Ubia huu una tija kwani utafungua uchumi wa kidijitali na kutengeneza
fursa za ziada kwa Watanzania.”
“Ushirikiano huu utaongeza kasi ya kuleta huduma za kifedha nchini, na
unaenda kuongeza nguvu kwenye kampeni yetu ya "Teleza Kidijitali"
inayolenga kuwafikia watu wengi nchini na huduma jumuishi za kifedha,”
aliongeza.
Mkurugenzi wa Fedha wa Vodacom Tanzania, Hilda Bujiku alisema: “Maoni
yetu daima ni kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa kidijitali na kubadilish
maisha kupitia teknolojia. Hivyo, ushirikiano huu unaenda sambamba na azma yetu
ya kuwafungulia wateja wetu fursa zinazobadilisha maisha.”
No comments:
Post a Comment