NAIBU Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa, amepokea taarifa kuhusu mpango wa Mgodi wa Kiwira-Kabulo unaomilikiwa na Shiriki la Madini la Taifa (STAMICO) kwa Mwaka wa Fedha 2023/24 ni kuzalisha Makaa ya Mawe yenye thamani ya shillingi bilioni 40.
Dkt.
Kiruswa amepokea taarifa hiyo kutoka kwa Mratibu wa Mgodi wa Kiwira-Kabulo
Mhandisi Peter Maha, wakati akiwasilisha taarifa ya mafanikio, changamoto na
mipango ya Mgodi katika Mwaka wa Fedha 2023/24.
Ili
kutekeleza hilo, Dkt. Kiruswa ameiagiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa
Madini Tanzania (GST) kushirikiana na STAMICO katika uchungizi wa sampuli za
Maabara hususan katika kuchunguza ubora wa Makaa ya Mawe.
Ametoa
maagizo hayo baada ya kutembelea mgodi wa Kiwira-Kabulo uliopo katika Kijiji
cha Kapeta Kata ya Ikinga wilayani Ileje mkoa wa Songwe ambapo amesema GST
tayari ina Ithibati inayotambulika Kimataifa hivyo Taasisi hizo mbili
zishirikiane kupima ubora wa Makaa hayo mgodini hapo ili kupunguza asumbufu kwa
wateja wanaotaka kupata vipimo kutoka Maabara zilizo thibitishwa Kimataifa.
Aidha,
Dkt. Kiruswa amesema, kutokana na uwekezaji mkubwa uliofanyika katika mgodi wa
Kiwira-Kabulo, ni vyema akatafutwa mwekezaji mkubwa Ili ashirikiane na STAMICO
katika uchimbaji wa makaa ya mawe ambapo kwa sasa yanahitajika kwa wingi katika
nchi mbambali duniani ili kuongeza uzalishaji na kuchimba kwa faida kwa lengo
la kunufaisha uchumi wa nchi.
Katika
hatua nyingine, Dkt. Kiruswa ameipongeza STAMICO kwa kuendelea kufanya vizuri
katika uzalishaji wa makaa ya mawe na kuendelea kuchangia huduma kwa jamii
zinazozunguka mgodi kama Sheria zinavyoelekeza na pia, amewasihi watumishi wote
kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kujitoa ili kuandika historia mpya kati ya
miradi ya STAMICO iliyofanikiwa.
Pia,
Dkt. Kiruswa ameahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali zinazoukabili mgodi
huo ikiwemo upungufu wa wafanyakazi, upungufu wa vitendeakazi, madai ya
watumishi na uchakavu wa majengo.
Kwa
upande wake, Mratibu wa Mgodi wa Kiwira-Kabulo Mhandisi Peter Maha amemshukuru
Naibu Waziri kwa kufanya ziara katika mgodi huo ambapo amesema kitendo hicho
kitaongeza morali ya kazi na kuchochea maendeleo ya uzalishaji katika mradi huo
ambao kwa kiasi kikubwa umefanikiwa kuendeleza uzalishaji wa makaa ya mawe na
kuhudumia soko la ndani na nje ya nchi.





No comments:
Post a Comment