NA
MAGENDELA HAMISI
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amewahakikishia
Watanzania kuwa watakwenda kwenye Uchuguzi Mkuu ujao huku vyama shiriki vikiwa na
maelewano makubwa.
Kinana alitanabaisha hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Mkutano Kitaifa wa Wadau, kujadili Hali ya Demokrasia nchini kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Katika Mkutano huo ambao umeandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Pia Kinana alifafanua kwamba kabla ya kuanza kwa mchakato wa Katiba Mpya, Asasi za kiraia zitatoa elimu kwa Watanzania kupitia yaliyomo kwenye Katiba ya mwaka 1977 ili kutoa dira ya kukamilisha hilo kabla ya uchaguzi ujao.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Chama na NCCR Mageuzi, Joseph Selasin, ameshauri kwamba ni vizuri uchaguzi wa Serikali za Mitaa na ukasimamiwa na Tume ya Uchaguzi badala ya kusimamiwa na Tamisemi kama ilivyo sasa.
“Nakumbuka mwaka 1995 tulifanya uchaguzi vizuri kwa kuwa tume iliajiri wafanyakazi wake na wapinzani tukafanya vizuri sana kwa maana tulifanikiwa kupata asilimia 40 ya kura na baada ya hapo tukashuka kutokana na kuwa chaguzi ya upande mmoja ni ni vema michakato hii ikafanyika kwa haraka,” amesema.
No comments:
Post a Comment