Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Tanzania (TTB), Mhe.Balozi Dkt. Ramadhan Dau (kushoto) akiwa katika kikao hicho.
Baadhi ya Wajumbe wa Menejiment ya TTB waliyohudhuria kikao hicho
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA.
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi Utalii Tanzania (TTB), Mhe. Balozi Dkt.Ramadhani Dau, ameanza rasmi kutekeleza majukumu yake kwa kukutana na Menejimenti ya TTB kwa lengo la kupata taarifa za bodi na kuweka mikakati ya kutekeleza majukumu aliyopewa.
Kikao hicho kimefanyika leo tarehe 22 Agosti, 2023 katika hoteli ya Gran Melia, jijini Arusha, ambapo mambo mbalimbali wameangalizia katika kufikia malengo ya bodi hiyo.
Kikao hicho leo Agosti 22, ni baada ya kuzinduliwa rasmi kwa Bodi hiyo jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa.
Balozi Dkt. Dau anaanza kazi hiyo baada ya kuteuliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt.Samia Suluhu Hassan, Agosti 5, 2023.
No comments:
Post a Comment