NA ANDREW CHALE, ZANZIBAR
TAMASHA kubwa la muziki wa Rege (Reggae) Zanzibar msimu wa tano ambalo limefanyika kwa siku mbili kwa Agosti 11 na 13,2023, Mambo Club ndani ya Ngome Kongwe, Unguja limefikia tamati usiku wa kuamkia leo huku waandaaji wakitangaza tarehe mpya ya msimu wa Sita kwa mwaka 2024.
Baada ya shangwe hiyo ya siku mbili, Mkurugenzi wa Tamasha hilo, Said Omary Hamad 'Side Rasta' ameishukuru watu wote waliojitokeza kushuhudia tamasha hilo pamoja na wadau wengine kwa namna ya kipekee ambavyo lifanyika kwa mwaka wa tano.
"Nawashukuru wasanii wote walipanda jukwaa la Mwaka huu la Zanzibar Reggae Festival. Wadau mbalimbali na wadhamini kwa ujumla shukrani kwa kujitokeza kwenu.
Mwisho wa tamasha hili ni mwanzo wa maandalizi ya tamasha la msimu unaofuata ambao utakuwa ni wa Sita na litafanyika Agosti 9 na 10, 2024 hapa hapa Ngome Kongwe." Amesema Side Rasta.
Aidha, amewaomba wadau kuendelea kujitokeza kudhamini tamasha hilo kuongeza fursa za kiuchumi.
Aidha, Wasanii mbalimbali wameweza kupanda jukwaa hilo ambapo kwa jana Agosti 12, Wasanii Hussein Masimbi kutoka Bagamoyo Tanzania, Grad Yahaya, Becky Muthoni (Kenya), Kush Riley (Jamaica).








No comments:
Post a Comment