AfisaUtamaduni Mkoa wa Mbeya
Victoria Shao akizungumza katika kikao maalumu kilichowahusisha Wasanii,
Waigizaji na waimbaji kilicho andaliwa na Wizara ya Utamadunim Sanaa na
Michezo.
............................................................
NA
MWANDISHI WETU, MBEYA
KIASI cha
Shilingi Bilioni 5, zimetengwa na Mfuko wa Wizara ya Sanaa na Utamaduni ili
kuwawezesha wasanii na waigizaji wa "Bongo Movie" wa Mkoa wa Mbeya.
Akizungumza
katika kikao maalumu kilichowahusisha wasanii, waigizaji na waimbaji wa mikoa ya
Mbeya na Songwe, Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa mfuko huo, Nyakaho Mahemba,
amesema wizara imeanza kutoa fedha hizo kwa wasanii kuanzia Desemba 2022 na
imelenga kukuza na kuendeleza kazi za wasanii kujiendesha kibiashara badala ya kuwa
burudani pekee.
Mahemba
amesema katika mpango wa Serikali ni kuongeza ajira na kuongeza mitaji kwa
wasanii kupitia mafunzo na kuongeza ubora wenye lengo la kukidhi soko la
ndani na nje ya nchi.
Amefafanua kuwa wasanii wana uwezo wa kukopa mtaji kuanzia sh. laki 2 hadi sh. Mil 100 ili kufikia malengo na kwamba Mfuko wa Utamaduni unashirikiana na mabenki ili kuwezesha mikopo ya wasanii.
Afisa Mtendaji
Mkuu, huyo ameendelea kusema kuwa tayari imeshatolewa mikopo kwa awamu mbili,
Desemba 2022 na mkopo wa pili umetolewa Februari ambapo tayari jumla ya sh.
bil 1.077 kwa miradi 45 na hivyo kuzalisha ajira 88,750.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni wa Mkoa, Victoria Shao, amesema mikopo hiyo ya wasanii itachangia ajira na kuwasaidia kuwainua kiuchumi ambapo wasanii,waimbaji,wabunifu wa kazi za mikono,waandishi wa kazi za kifasihi na wachoraji wanapaswa kuchangamkia fursa hiyo.
Shao
amesema serikali itakuwa karibu na wasanii kwa maelekezo na elimu ya mikopo ili
waweze kukopa kurejesha ili iweze kuwanufaisha wasanii wengine.








No comments:
Post a Comment