WAZIRI BASHUNGWA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA UJENZI DARAJA LA SUKUMA LENYE UREFU WA MITA 70 JIJINI MWANZA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Sunday, December 17, 2023

WAZIRI BASHUNGWA ASHUHUDIA UTIAJI SAINI MKATABA UJENZI DARAJA LA SUKUMA LENYE UREFU WA MITA 70 JIJINI MWANZA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa(Mb) akishuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Sukuma lenye urefu wa mita 70 na barabara unganishi ya kilometa 2.294 kwa kiwango cha lami, kati ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta na Kampuni ya Mumangi Construction Company Ltd, Mhandisi Nyangureta Mumangi, leo tarehe 17 Disemba 2023 Wilayani Magu jijini Mwanza.

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta na Mkurugenzi Mzawa wa Kampuni ya Mumangi Construction Company Ltd, Mhandisi Nyangureta Mumangi wakionesha Mkataba wa ujenzi wa daraja la Sukuma lenye urefu wa mita 70 na barabara unganishi ya kilometa 2.294 kwa kiwango cha lami mara baada ya kusaini mkataba huo mbele ya Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa(Mb), leo tarehe 17 Disemba 2023 Wilayani Magu jijini Mwanza.

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa(Mb) (kulia) akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ng'wilabuzu Ludigija katika hafla ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa daraja la Sukuma lenye urefu wa mita 70 na barabara unganishi ya kilometa 2.294 kwa kiwango cha lami, leo tarehe 17 Disemba 2023 Wilayani Magu jijini Mwanza.


No comments:

Post a Comment