MAOFISA HABARI WATAKIWA KUTANGAZA MIRADI YA SERIKALI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, February 28, 2024

MAOFISA HABARI WATAKIWA KUTANGAZA MIRADI YA SERIKALI


1Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Damas Ndumbaro akizungumza na maafisa Mawasiliano Serikalini wakati wa akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha Tarehe 27 Februari,2024.

NA MWANDISHI WETU

 MAOFISA Habari Serikalini wameagizwa  kutangaza miradi na shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili wananchi wajue ikiwemo  kujibu hoja za uongo zinazotolewa na watu dhidi ya serikali .


Akifungua Mkutano wa siku tatu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano Serikalini(TAGCO) Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo ,Dk,Damas Ndimbaro kwaniaba ya Naibu Waziri Mkuu,Doto Biteko.


Alisema maofisa hao wanawajibu mkubwa wakutangaza shughuli mbalimbali zinazofanywa na serikali ili watu waone ukubwa wa kazi zinazofanywa na serikali katika nchi hii


"Baadhi ya watu hawaoni ukubwa wa katarasi nyeupe ulivyo sasa ni wajibu wenu kueleza kazi zinazofanywa na serikali ikiwemo kujibu hoja za uongo dhidi ya serikali lazima mjue kujibu fitna na zengwe"


Alisema hata serikali inapigwa fitna sasa ni kazi yenu kujibu fitna na zengwe kwani hivi sasa zama za teknolojia ya habari imekua na ni nzuri ila inachangamoto zake kupitia mitandao ya kijamii.


Alisema mojakati ya changamoto kubwa iliyoletwa na mitandao ya kijamii haijui ni nani mtoa habari na nani anayepaswa kujua hii ni habari hivyo tumieni changomoto hizi kwaajili ya kujibu hoja na lazima mafunzo ya mara kwa mara yatolewe ya matumizi ya mitandao ya kijamii


"Ongezeni ubunifu zaidi,msifanye kama jana kazi zenu maafisa habari ili muweze kupambana zaidi na kuipambania serikali "


Alitoa rai kwa waandishi wa habari vyombo vya  serikali na maafisa habari  kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa uzalendo,weledi na ubunifu pale taarifa zinavyoandikwa


Alitoa maelekezo kwa waaajiri wote wasioweza kuleta maafisa habari kushiriki mkutano huo watoe maelezo kimaandishi na ifikapo mwakani Maafisa wote wa serikali na wasio wa serikali wajiunge na chama hicho


Alisema treni ya majaribio ya umeme imeanza kazi kwa majaribio ingawa kulikuwa na kebehi nyingi sana lakini treni imeshaanza kazi hivyo serikali inafanya kazi kwa vitendo


Aliwasihu maafisa hao kujiunga kwa pamoja kutetea serikali pale jambo linapotokea badala ya kuachia wizara husika pekee kutoa ufafanuzi ikiwemo kutoa hamasa kwa wananchi kujua umuhimu wa zoezi la uchaguzi wa serikali za mitaa ikiwemo utangazaji wa miradi ya kimkakati ya serikali 


Huku  Msemaji Mkuu wa Serikali,Mobhare Matinyi alisema baadhi ya halmshauri hazina maafisa mawasiliano wa serikali badala yake maofisa Tehama ndio wanaongoza kitengo hicho hali inayokwamisha hali ya wananchi kupata habari.


"Halmashauri 180 zilizopo nchini lakini inashangaza kuona baadhi yao siwezi kutaja idadi hazina maafisa habari na hawajui maana ya habari na ukiuliza sababu gani hakuna maafisa habari unajibiwa majibu yasiyorithisha"


Lakini pia kwenu maafisa mawasiliano ya serikali wapeni nafasi nao wananchi wazungumze kuhusu mambo mbalimbimbali yanayowasibu ila pia ni lazima sasa halmashauri ziajiri maafisa habari ili waweze kusemea vema serikali na wananchi kupata habari zaidi


Naye Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari na Teknolojia na Mawasiliano, Selestine Kakere alisema wizara inatekeleza kutangaza sera,kanuni na taratibu ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali ambapo kazi za serikali kwa Umma zinafanyika kupitia mitandao ya kijamii,radio na luninga


Alitoa rai kwa baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya ambao mikoa yao Haina maofisa habari wafanye hima kuajiri maofisa habari katika mikoa yao stahiki


Alisema mikoa 14 imepata fursa ya kutangaza miradi mbalimbali ya serikali huku zoezi hilo likiwa linaendelea ikiwemo uwekaji misingi ya uhuru wa vyombo vya habari sanjari na kushamiri kwa idadi kubwa ya vyombo vya habari ikiweo magazeti ,radio na televisheni za mitandao,blogu .


Alisema uwepo wa baadhi ya Wanahabari wengine wasio na weledi na sifa za wanahabari lakini bodi ya ithibati ipo katika hatua ya uanzishwaji ili kusaidia kuimarisha weledi katika sekta ya habari nchini  huku baadhi ya taasisi za  mawasiliano kwa umma baadhi hazitekelezi majukumu yake.


Naye Mkuu wa Wilaya ya Monduli,Joshua Nassari alisema ushirikoshwaji wa maofisa mawasiliano ni chachu ya kutoa taarifa kwa umma na kuongeza kuwa wamepokea agizo lakila halmashauri kuwa na maofisa habari na mikoa kwa ujumla


Awali Kaimu Mwenyekiti wa TAGCO,   Karim  Meshack alisema chama hicho kitaendelea kuhakikisha kinawunganisha maafisa habari kujadili mambo mbalimbali sanjari na kujifunza mbinu mbalimbali za teknolojia za upashanaji habari.

 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Selestine Kakele akitoa neno la utangulizi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika kwenye ukumbi wa AICC Jijini Arusha 



Baadhi ya Washiriki wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia majadiliano ya mada ya kwanza iliyohusu Crisis Communication Turning Challenges into Oportunity.


 Msemaji Mkuu wa Serikali Mobhare Matinyi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha Tarehe 27 Februari,2024


Msimamizi wa Majadiliano ya Mkutano Mkuu wa TAGCO, Bakari Machumu ambaye ni Mkurugenzi wa Mwananchi Communication akiteta jambo na Anastazia Rugabwa Mkurugenzi wa Ushawishi na Ushirikishwaji kutoka Twaweza East Afrika wakati wa majadiliano ya mada iliyohusu Crisis Communication Turning Challenges into Oportunity.

Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Damas Ndumbaro (Katikati) akionyesha Jarida la TAGCO mara baada ya kulizindua wakati wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha Tarehe 27 Februari,2024 na kushoto kwake ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Joshua Nasari.



Katika picha ya pamoja ni Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Damas Ndumbaro (Katikati aliyekaa) na maafisa habari wa Mamlaka za Serikali za Mitaa mara baada ya ufunguzi wa ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali (TAGCO) uliofanyika kwenye Ukumbi wa AICC Jijini Arusha Tarehe 27 Februari,2024

No comments:

Post a Comment