TEMBELEENI VIVUTIO VYA UTALII - TANAPA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Monday, February 26, 2024

TEMBELEENI VIVUTIO VYA UTALII - TANAPA


NA ANDREW CHALE, SAADAN

MAMLAKA ya Hifadhi ya Taifa imewataka Watanzania kujitokeza kutembelea vivutio vya utalii ili kuongeza mapato ya ndani.

 

Wito huo umetolewa na Kamanda wa   Uhifadhi wa Kanda ya Mashariki, Gibril Mwishawa, (Februari 25, 2024), ambapo amewataka kuwa na utamaduni wa kutembelea hifadhi zilizopo nchini.


Mwishawa amesema Tanzania ina utajiri wa hifadhi na Tanapa wana Kanda nne za kiutawala kwa Kanda ya Mashariki ambazo ni Saadan, Nyerere, Mikumi na Udizungwa.


Akizungumza kuhusu hifadhi ya Sadaan ambapo wamefanya Tamasha la kuhamasisha utalii lililopewa jina la Aura 2024, alisema hifadhi hiyo ni muhimu kwa sababu ya kuwa na vionjo vya mbuga na bahari.


Alitaja sababu nyingine ya Watanzania kutembelea hifadhi hiyo kuwa ni kuchangiwa na kutembelewa zaidi na watalii na wageni, kama ilivyo kwa zile za Kaskazini.


Katika kuhakikisha hilo linakamilika amesema tayari wameshaainisha maeneo ya uwekezaji na yameshatumwa maombi mbalimbali ikiwemo na hifadhi ya Saadan kwa lengo la kusaidia kukuza utalii katika Hifadhi za Kanda za Mashariki.


Naye Kamishna msaidizi wa Maendeleo ya biashara Tanapa Jully Lyimo, akizungumzia kuhusu Sadaan alisema ni eneo zuri kwakuwa lina vivutio vya utalii wa kupanda gari, kuona wanyama, utalii wa kutembea, utalii wa usiku, utalii wa fukwe na boti.


Lyimo alitoa wito kwa Watanzania kutumia hifadhi hiyo ya Saadan, kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kipaimala, harusi na sherehe nyingine.


Hifadhi ya Saadan ina asilimia 70 katika hifadhi ya Saadan ni eneo la nchi kavu na asilimia 30 ikiwa ni eneo la bahari ya hindi huku kukiwa na wanyama wakubwa wanne (Big four) tembo,twiga, chui, simba, lakini pia viboko na wanyama wengine .




No comments:

Post a Comment