Kiongozi wa Chama ACT Wazalendo Dorotty Semu.
NA MAGENDELA HAMISI
CHAMA Cha ACT Wazalendo, kimetangaza Baraza jipya la Mawaziri kivuli likiwa ni la pili tangu kuanzishwa kwa chama hicho na kulipa majukumu tisa ya kuanza nayo kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi.
Akizungumza awali na baada ya kutangaza baraza hilo leo Machi 20,2024 Kiongozi wa chama hicho, Dorotty Semu, amesema tangu kuanza kwa baraza hilo ambalo lengo lake lilikuwa ni kuisimamia Serikali baada ya matokeo ya uchaguzi wa 2020 kukosa uwakilishi mzuri bungeni.
Ameongeza kuwa kwa miaka miwili iliyopita baraza hilo limekuwa na nguvu ya kuyasemea na kuishauri Serikali kuhusu masuala mbalimbali ambayo yamekuwa kero kwa wananchi ikiwemo migogoro ya ardhi, madai ya wafanyakazi, suala la kupanda kwa gharama za maisha.
Masuala mengine waliyafanyia kazi katika kipindi cha miaka miwili iliyopita ni mahitaji ya bima ya afya kwa watanzania wote na masuala ya bei na vyakula na mazao na kusababisha baadhi ya hoja kufanyiwa kazi na Serikali.
“Baadhi ya hoja ambazo zilifanyiwa kazi na Serikali ni kuhusu tozo za miamala, kuondolewa kodi kwenye mafuta ya kula,NRFA kuwezeshwa na Serikali kununua chakula ili kupunguza gharama za chakula nchini na masuala hayo yamefanya baraza kivuli la ACT Wazalendo kuwa sauti kuu ya Chama katika kukosoa Serikali na kupendekeza sera mbadala, amesema.
Pia amesema baraza kivuli la ACT Wazalendo limekuwa jukwaa la kufunda viongozi wapya wa chama hicho na kuwajenga na kuwatengeneza kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwa kuzingatia jinsia na kusisitiza chama hicho kitaendelea kuwa kiongozi kwa kufanya siasa mpya zinazojali maslahi ya taifa na zinazotoa majawa kwa masuala ya wananchi.
Aidha amesema baraza jipya mambo tisa yatakayoanza nayo ni kuendelea kupigania kupatikana kwa unafuu wa gharama za maisha kwa wananchi kwa kutoa mapendekezo ya kudhibiti kupanda kwa bei za vyakula nchini.
Jambo la pili, wataishinikisha Serikali kupunguza bei za
nauli za mabasi yaendao mikoani na daladala, lingine ni kuwahakikishia wananchi
kuhusu upatikanaji umeme wa uhakika, kupigania haki za usalama wa ardhi kwa
mijini na vijini jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa.
Ameongea kuwa baraza hilo pia litakuwa na jukumu la kulizungumzia na kupeleka maoni kwa Serikali kuhusu vikokotoa kwa wastaafu jambo ambalo limekuwa ni kilio kwa wataafu wengi na kusababisha hata wanaoekelea kustaafu kuwa na hofu ya maisha yao baada ya hapo kama kweli wataweza kumudu hali ya maisha.
Tofauti na amesema kuwa baraza litakuwa na jukumu la kuhakikisha inapigia kelele masuala ya ubadhirifu na kuifanyia kazi ipasavyo kiuchambuzi taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CIG) ili wanaotawajwa kuhusika na ubadhilifu wafikishwe kwernye vyombo vya sheria ili hatua zichukuliwe dhidi hyao.
Pia kuzifanyia kazi ipasavyo taarifa za wananchi na kuishauri Serikali kuhusu kundi kubwa la vijana ambao wanamaliza vyuo na kukosa ajira, hivyo ni vema sasa kuwe na mpango mahususi wa kuhakikkisha ajira zinapatikana kwa wingi kwa kundi hilo.
Akitangaza baraza hilo kivuli, ametanabaisha kuwa Isihaka Mchinjita atakuwa Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi ni Idrisa Abdul.
Waziri wa Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana, Kazi na Ajira ni Ndolezi Petro Ndolezi na naibu wake ni Salma Mbarouk Abdallah, Waziri wa Ofisi ya Rais Mipango, Fedha na Hifadhi ya Jamii ni Kiiza Mayeye, naibu wake ni Shangwe Ayo.
Waziri wa Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora ni Riziki Shahali Mngwali , naibu wake ni Seif Hamad Sulemani, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo Vijijini ni Kuruthumu Jummane Mtutuli, naibu wake ni Hussein Juma.
Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano ni Pavu Juma Abdallah na naibu wake ni Revocatus Setembo, Wizari ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inashikiliwa na John Patric Mbozu na naibu wake ni Hadija Anwar Mohammed.
Kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imetwaliwa na Daria Majid Hassan na naibu wake ni Juma Hamd Kombo, Wizara ya Katiba na Sheria inashikiliwa na Mbarara Maharagande huku Naibu wake akiwa ni Amir H. Kaswaka.
Katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki inashikwa na Dkt. Nassoro Omari huku naibu wake ni Mhidini Thabiti Nkwera, kwenye Wizara ya Afya ni Elizabeth Sanga na naibu wake ni Rukaya Mohammed Nasri.
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi inakamatwa na Wakili Emmanuel Mvula na naibu wake ni John Safari, katika Wizara ya Kilimo na Umwagiliaji na Maendeleo ya Ushirika ni Mtutula Abdallah Mtutula, naibu wake ni Julius Joseph Masabo.
Hamidu Bobali ni Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia huku naibu wake ni Makaranga Ntebe, Waziri wa Nishati ni Filbert Simon Macheyeki naibu waziri wake ni Shuwena Faki Haji, Waziri wa Rasilimali na Migodi ni Edgar Francis Mkosamali , naibu wake ni Rai Ibrahimu Hamis.
Wiziri wa Miundo Mbinu ni Mhandisi Mohammed Mtembo huku naibu wake ni Fidel Christopher, Waziri wa Maji ni Yasinta Cornel naibu wake ni Stanley Mbembachi, Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi ni Seleman Sango na naibu wake ni Marijani Rajab Ndandavale, Waziri wa Habari na Mawasiliano na Tehama ni Rahma Mwita.
Waziri wa Viwanda na Biashara ni Mwanaisha Mdeme naibu wake ni Felix Kamugisha, Waziri wa Maliasili ni Julian Mwakangali na naibu wake ni Anton Shika, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Waziri wake ni Ebiro Wakazi Wasira naibu wake ni Monalisa Joseph Ndalla.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wanawake na Makundi Maalum ni Janel Joel Richard na naibu wake ni Juster Denis Selestine.





No comments:
Post a Comment