TANAPA YAFANIKIWA KUDHIBITI UJANGILI NA KUONGEZA WATALII NCHINI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Thursday, March 21, 2024

TANAPA YAFANIKIWA KUDHIBITI UJANGILI NA KUONGEZA WATALII NCHINI

Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Kuji, akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari jijini dar es Salaam leo, Machi 21, 2024 kuhusu mafanikio ya shirika hilo kwa kipindi cha miaka mitatu.

NA MAGENDELA HAMISI

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limesema kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani wamefanikiwa kudhibiti ujangali ambao ulikuwa tishio nyakati za nyuma na pia kuongeza idadi ya watalii nchini.

Hayo yamesemwa na leo Machi 21, 2024 jijini Dar es Salaaam na Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Musa Kuji wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kufafanua kuwa kwa mawaka 2018/19 watalii waliotembelea Hifadhi za Taifa ni 1, 452, 345 ikijuishwa watalii wa ndani 719,172 na wanaotoka nje ni 733,173.

Ameongeza kuwa baada ya jitihada kadhaa kufanywa na Rais Samia matunda yakaanza kuonekana kwa mwaka 2022/23 watalii 997,873 kuja nchini na kutembelea hifadhi na mwaka 2022/23 wakawa 1,670, 437.

Amefafanua kuwa kwa mwaka 2023/24 Machi tayari watalii 1,514,726 wamembelea hifadhi wa ndani wakiwa 721, 543 na kutoka nje ni 793, 183 sawa na ongezeko la asilimia tano ikiwa ni zaidi ya malengo ambayo walijiwekea ya kupokea watalii 1,387, 987.

“Hivyo tayari tumekusanya shilingi bilion 340 na makadilio hadi kipindi cha mwisho wa mwaka wa fedha ambapo tumebakisha robo naamini tutakuwa tumekusanya sh. bilion 380 na katika kipindi cha miaka mitatu ijayo hakika hatukuwa hapa na yote yametokana na kufanya vizuri kwa filamu ya Royal Tour,” amesema.

 Pia amesema kuwa atayafanyia kazi mawazo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile kuhusu maziko ya viongozi wakuu (marais) yawe TANAPA kama inavyofanyika kwa mataifa mengine duniani.

Naye Naibu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Herman Batiho amesema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu kwa ni jambo jema kuona wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhibiti ujangili wa wanyama faru, tembo, samba na wengineo na kusababisha kuongezeka wanyama kwenye hifadhi mbalimbali nchini.

“Binafsi hatuwezi kutaja idadi ya wanyama ambao wameongezeka kwa kuwa ipo taasisi ambayo imepewa jukumu la kufanya utafiti na kutangaza hivyo tusubiri muda ukifika watatangaza idadi ya wanyama ambao wameongezeka kwa kipindi cha miaka mitatu.

Akizungumzia changamoto ya kutoweka kwa shoroba nyingi na kubaki chache, amesema kuwa hilo ni tatizo kubwa na inatokana na kuongezeka kwa idadi ya watu nchini na kusababisha kuingilia maeneo ya wanyama.

“Kwa mwaka 1970 shoroba zilikuwa saba na sasa zimebaki tatu na baada ya kufanyika kwa tafiti imebainika sababu kubwa na kungezeka kwa watu na kama  shirika tumekaa na Wizara husika tayari jitihada zinachukuliwa ili kudhibiti kutoweka kwa shoroba, amesema.

Pia Kamishna Msaidizi Uhifadhi TANAPA, Mhandisi Dkt Richard Matolo, akizungumzia suala la ujenzi wa Hoteli ya nyota tatu ndani ya hifadhi ya Burigi Chato amesema kuwa kwa sasa ipo katika hatu ya awali ya ujenzi ambao unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu.

“Kujenga kwa hoteli katika mbuga ya Burigi Chato ni mpango mkakati wa ,kuongeza watalii jatika mbuga hiyo na haukuja kwa kurusha shilingi bali ilifanyika tathimini ya kina na ikaamliwa ijenge kule,” amesema.

Ameongeza kuwa hoteli hiyo itakuwa na vyumba vikubwa ‘King size’ vitakavyokuwa na huduma nyingi tofauti na inavyosemwa na baada ya kukamilika kwa ujenzi wa awali itafuata awamu ya pili ina vyumba 30.

Naibu Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Herman Batiho

       Kamishna Msaidizi Uhifadhi TANAPA, Mhandisi Dkt Richard Matolo




No comments:

Post a Comment