BODABODA 32 ZA WIZI ZANASWA, 13 ZATAMBULIWA WATUHUMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, March 5, 2024

BODABODA 32 ZA WIZI ZANASWA, 13 ZATAMBULIWA WATUHUMIWA KUFIKISHWA MAHAKAMA


NA MAGENDELA HAMISI

JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa wizi wa pikipiki, Omari Kopa (28) mkazi wa Mlandizi na wenzake wawili wakiwa na pikipiki 32 ambazo zimeibwa katika maeneo mbalimbali jijini humo na mikoa ya jirani.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro, amesema kwamba watauhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote baada ya taratibu za kisheria kukamilika na kuweka wazi kuwa kati ya pikipiki hizo 13 tayari zimetambuliwa na wamiliki.

“Watuhumiwa wengine wanaendelea kutafutwa na wakipatikana watafikishwa mahakamani na ninatoa wito kwa waliobiwa pikipiki ambao bado hawajaziona wafike katika vituo vya Polisi vya Kigamboni, Mbagala na Chang’ombe wakiwa na vielelezo vyao vya umiliki ili kukagua zilizokamatwa kama ni zao,” amesema.

Ameongeza kuwa Jeshi hilo kupitia Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Feb sita mwaka huu lilianza Operesheni kubwa ya kuzuia vitendo vya kiarifu ambavyo vinavyoonekana kuendelea kushamili hususan kwenye wizi wa pikipiki na kufanikiwa kukamata pikipiki hizo na watuhumiwa hao.

Kamanda Murilo, amesema tofauti na hilo tangu Feb mwaka huu na wanaendelea kuendesha operesheni kufuata sheria barabarani na kubaini waendesha pikipiki hususan bodaboda wamekuwa na makosa mengi ikiwemo kutozingatia taa za barabarani na vivuko vya waenda kwa miguu.

“Kundi hilo la waendesha bodaboda ambao hawafuati sheria wengi wao tumewakamata na kuwafikisha mahakamani baadhi yao wamelipa faini na mmoja anatumikia kifungo na mashauri saba bado yapo katika ofisi ya mashtaka.

“Makosa ambayo yamekuwa yakijirudia ni kutovaa kofia, kutozingatia taa za barabarani, kupakia abiria zaidi ya mmoja , mwendokasi ambao unawasababishia ajali na kuharibu mali ikiwemo pikipiki hizo, hivyo Jeshi la Polisi linaendelea kutoa elimu kwa madereva wa vyombo hivyo na tunaendelea na Oparesheni ili kuhakikisha sheria inazingatiwa na tutakaowakamata tutaiuliza sheria ili ituongoze kuchukua hatua,” amesema.

Thobius Christpher, mkazi wa Kimara, Dar es Salaam ambaye pikipiki namba MC 456 iliibiwa Aprili 17, 2022 analishukuru Jeshi la Polisi Kanda ya Dar es Salaam kwa kufanikisha kupatikana kwa bodabidfa yake ingawa ikiwa katika hali ya uchakavu.

"Pikipiki yangu iliibiwa maeneo ya Mlimani City jijini Dar es Salaam na sikutegemea kama ningeipata, hivyo nalishukuru Jeshi la Polisi kwa kufanikisha kuipata," amesema 





No comments:

Post a Comment