RAIS SAMIA KUANZA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, March 5, 2024

RAIS SAMIA KUANZA KUSIKILIZA KERO ZA WANANCHI

 


NA MAGENDELA HAMISI

KATIKA kuenzi kwa vitendo nyendo za hayati, Rais mstaafu wa awamu ya pili Alli Hassan Mwinyi , Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, naye amepanga kuanza kukutana na wananchi kusikiliza kero zao kwa lengo la kutathimini kazi za watendaji wake katika kuwahudumia watanzania.

Imeelezwa kuwa Rais Samia atakuwa akitumia siku moja kila mwezi kuzungumza na wananchi katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar na atafanya hivyo bila kujali itikadi, dini waka kabila.

Hayo yamebainishwa leo, Feb 5, 2024 jijini Dar es Salaam na Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mfunzo wa CCM, Paul Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara aliyofanya katika mikoa 23 na kufafanua kuwa sasa kiama kwa watumishi wa umma kimefika.

”Nitume salamu kwa watumishi ambao kero zao zimefIkishwa ofisini na hawajazitatua, pindi zitakapofikishwa kwa Rais ni dhahiri kiama chao kitakuwa mlangoni,” amasema Makonda.

Akiweka wazi kuhusu ziara yake, Makonda amesema amebaini mambo mengi ikiwemo dhuluma kwa baadhi ya watanzania kuumizwa na kama chama wanawajibu wa kuishauri Serikali ili kupambana na hilo ili kupata utatuzi wa changamoto hiyo ambayo haipaswi kufumbiwa macho kwa maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa baadhi ya mambo ambayo amebaini tayari ameyafikisha kwa Katibu Mkuu wa Chama na yanafanyiwa kazi na mengine yalishanyiwa kazi hapo kwa hapo akiwa ziarani, yaliyokuwa chini ya uwezo wake.

Amesema wananchi wengi wamedhulumiwa ardhi na tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa kudhibiti changamoto hiyo na kutoa funzo kwa watu wanaotumia fedha zao vibaya kudhurumu ardhi za wanyonge.

“Nadhani Waziri husika anapaswa kufanya mapitio kwa watendaji ambao wameweka minyororo ya utapeli kwa maana inaonekana kuna mtandao mkubwa katika sekta hiyo na kusababisha watu wasiokuwa na uwezo kudhulumiwa ardhi, hivyo ni vizuri hatua kali zichukuliwe kwa watakaobainika,” amesema .


No comments:

Post a Comment