CHUO Cha Furahika kimeanza kutoa kozi ya usomaji mita za maji ‘Water Meter’ kwa wanafunzi ambao wamemaliza kidato cha nne na hawakupata alama nzuri za kuendelea na kidato cha tano.
Akizungumza na waandishi wa habari katika chuo hicho chenye usajili wa namba VET/DSM/PR/2021/169 kilichopo Malapa – Ilala jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkuu wa Chuo hicho, Dkt David Msuya amesema, wanaendelea na usajili wa wanafunzi kwa kozi ya Hotel, Bandari, IT Sekretari na nyinginezo na wanafunzi watagharamia vifaa vya kujisomea pekee.
Akizungumzia kozi ya usomaji mita za maji, Dkt. Msuya amesema lengo lake kuhakikisha wanazisaidia Mamlaka za Maji nchini kuwa na wataalamu wa kutosha katika eneo ambalo linahitaji wafanyakazi za wengi sili kuleta ufasi kwenye sekta hiyo.
“Ninawaombe wazazi walete vijana wao hapa ambao wamemaliza kidato cha nne na hawakupa alama stahiki za kuendelea na masomo ya kidato cha tano ama kuwa na sifa ya kujiunga na vyuo vingine vya elimu ya juu hapa nchini,” amesema.
Ameongeza kuwa kozi hiyo ya usomaji mita itatolewa kwa kipindi cha miezi sita na mwaka mmoja na mwisho wa kupokea maombi ya wanafunzi kwa ajili ya kuanza muhula wa masomo inatarajiwa kuwa ni Machi 17 mwaka huu.
Wakati huo huo, Dkt Msuya amesema kwamba katika kozi za Hotel wanazo nafasi za kazi kwa ajili walimu wa kike pekee ambazo uwezo wa kufundisha na kiwango chao cha elimu wawe na Diploma huku wenye elimu ya Cheti anaweza kufikiliwa kulingana na uwezo wake wa kufundisha.
“Ukiachana na kuwahitaji ealimu hao kwa kozi ya Hotel, pia tunazo nafasi kwa walimu wa kujitolea katika masomo ya Bandari na Biashara tunawakarubisha kwa ajili ya kuendeleza ujuzi wao ili kujitengenezea CV ili kujiweka sawa katika harakati za kutafuta ajira,” amesema.
No comments:
Post a Comment