UONGOZI wa Chuo
cha Ufundi Stadi cha Furahika chenye namba za usajili VET/DSM/PR/2021D169 ambacho
kipo Buguruni Malapa – Ilala jijini Dar es Salaam, umesema kuwa wanawahitaji
madereva wastaafu kwa ajili ya kuongeza nguvu chuoni hapo.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake, Machi 3, mwaka huu Kaimu Mkuu wa Chuo hicho,
David Msuya amesema lengo la kuwahitaji madereva hao ni kwaajili ya kutoa
mafunzo ya fani hiyo kwa wanafunzi wao.
“Tunaamini
kwamba madereva ambao wamestaafu watakuwa na busara, ujuzi na maarifa makubwa
katika kuwafundisha vijana wetu wanaokuja hapa chuoni kwa ajili ya mafunzo ya
udereva na watakapomaliza mafunzo naamini watakuwa wameiva kwelikweli na wataweza
kufanya kazi popote,” amesema.
Ameongeza kuwa
sifa nyingine ni vema dereva huyo awe na umri kuanzia miaka 60 na kuendelea na
hata wale ambao waliacha kazi kwa sababu mbambali na kwa na uzoefu wa kutosha,
asisite kupeleka maombi ya kazi katika chuo hicho.
Pia amesema
wanaendelea kusajili wanafunzi kwa ajili ya kozi mpya ya Usomaji Mita za Maji ‘Water
Meter’ na mwisho wa kupokea maombi ni Machi 17 mwaka huu.
Tofauti na hilo,
Dkt Msuya amesema chuo chake kinahitaji walimu wa kujitolea kwa wanaoweza
kufundisha kozi ya Bandari, Biashara na
zaidi walimu wake kike watapewa kipaumbele.
“Pia tunahitaji
walimu wa masomo ya Hoteli, sifa awe na Diploma huyo tutampa makataba wa ajira
hivyo wenye sifa tunawakaribisha,” amesema.





No comments:
Post a Comment