
NA MAGENDELA HAMISI
magendela@gmail.com-
0718594040
TANZANIA imepokea
vidonge vya matone vitamin A, milioni 22 vyenye thamani ya shilingi bilioni 99 kutoka
katika Shirika la Nutrition Internation (NI) la Canada kwa ajili ya chanjo kwa
watoto chini ya miaka 5.
Pia imeemwa
kuwa katika mchakato huo watoto milioni 11 watapatiwa chanjo kwa awamu mbili June
na yapili itafanyika Desemba itakayowasaidia kuondokana na udumavu, kuhimalisha
afya ya macho na kinga ya mwili.
Vidonge vya
matone ya Vitamini A, vimekabidhiwa leo Machi 13 jijini Dar es Salaam na Mjumbe
wa Bodi wa shirika hilo, Dkt Jakaya Kikwete ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu
ya Nne wa Tanzania na amesema licha ya kukabidhi vidonge hivyo taifa bado
linakabiliwa na watoto wenye udumavu kwa asilimia 30.
“Wakati
nilipoingia madarakani nilikuta ni asilimia 42 ya watoto wenye udumavu ,
tukajihidi kuisukuma na nilipotoka 2015 tukaaacha 34 na sasa imekuwa 30 lakini
bado tuko chini sana kwa maana kuwa na watoto asilimia 30 wenye udumavu ni tatizo.
Kwamba uzito wao haufanani na umri wao kuna
ukondefu pia tatizo kubwa ni upungufu wa damu ‘Anemia’ na kwa takwimu ambayo
imetolewa na daktari zinatisha kwani asilimia 59 na zaidi ya watoto chini ya miaka
mitano na akina mama wajawazito vifo vyao vinatokana na changamoto hiyo,”
amesema.
Ameongeza
kuwa baada ya vidonge hivyo kutolewa na kusambazwa nchini anaamini itasaidia kupunguza
changamoto hiyo na kuhimalisha afya wa watoto hao na muhimu kwa wazazi
kuhakikisha watoto wanapatiwa matone hayo.
Aidha, amesema Shirika la NI, limetoa vidonge milioni 500 duniani kote na Tanzania imepata vidonge milioni 22 kulingana na idadi ya watoto walipo nchini ambao ni milioni 22.
N a kutokana
na changamoto hiyo kujitokeza mwaka 2021 walifanikiwa kutoa chanjo ya vitamin A,
124 na kusaidia kuzuia vifo vya watoto milioni 32 duniani na katika kipindi
hiki wamefanikiwa kuokoa vifo vya watoto milioni saba.
Pia Mkuu wa
Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Albert Chalamila, amesema kutokana na kuelewa umuhimu wa matone hayo
watahakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kufanikisha mchakato
huo kwa asilimia kubwa.
Kwa upande
wake, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel
amesema elimu ya mtoto inaanza siku mimba inapotunga na sio shuleni kwa
kumpatia Mama lishe ili bora wakati wa ujauzito itakayosaidia kuimarisha ubongo
wa mtoto.
Hivyo,
ametoa wito kwa jamii hususan wazazi kuzingatia Lishe Bora kwa tangu mimba
inapotungwa kwa lengo la kusaidia mtoto atakayezaliwa kuwa na afya njema hadi
anapofikia hatua ya kuanza shule atakuwa na uelewa mzuri darasani.
Mwakilishi wa Balozi wa Canada hapa nchini, Helen Fytche akizungumza.
ProperNutritionis your first defense against illness and fatigue.
ReplyDeleteGood Nutrition
ReplyDeletestarts with mindful grocery shopping and home-cooked meals.
From macro tracking to recipe suggestions, AI reshapes Nutrition with ease.
ReplyDeleteHealthy living has officially entered the AI era.