NUTRITION INTERNATIONAL YAIKABIDHI TANZANIA VIDONGE VYA VITAMINI A KWA AJILI YA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, March 13, 2024

NUTRITION INTERNATIONAL YAIKABIDHI TANZANIA VIDONGE VYA VITAMINI A KWA AJILI YA WATOTO CHINI YA MIAKA MITANO

 

Mjumbe wa Bodi ya Nutrition International, ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Dkt Jakaya Kikwete (katikati) na Mwakilishi wa Balozi wa Canada hapa nchini, Helen Fytche, wakimkabidhi, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, (kushoto) moja ya boksi lenye vidonge vya vitamini A. 

NA MAGENDELA HAMISI

magendela@gmail.com- 0718594040

TANZANIA imepokea vidonge vya matone vitamin A, milioni 22 vyenye thamani ya shilingi bilioni 99 kutoka katika Shirika la Nutrition Internation (NI) la Canada kwa ajili ya chanjo kwa watoto chini ya miaka 5.

Pia imeemwa kuwa katika mchakato huo watoto milioni 11 watapatiwa chanjo kwa awamu mbili June na yapili itafanyika Desemba itakayowasaidia kuondokana na udumavu, kuhimalisha afya ya macho na kinga ya mwili.

Vidonge vya matone ya Vitamini A, vimekabidhiwa leo Machi 13 jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Bodi wa shirika hilo, Dkt Jakaya Kikwete ambaye pia ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Tanzania na amesema licha ya kukabidhi vidonge hivyo taifa bado linakabiliwa na watoto wenye udumavu kwa asilimia 30.

“Wakati nilipoingia madarakani nilikuta ni asilimia 42 ya watoto wenye udumavu , tukajihidi kuisukuma na nilipotoka 2015 tukaaacha 34 na sasa imekuwa 30 lakini bado tuko chini sana kwa maana kuwa na watoto asilimia 30 wenye udumavu ni tatizo.

 Kwamba uzito wao haufanani na umri wao kuna ukondefu pia tatizo kubwa ni upungufu wa damu ‘Anemia’ na kwa takwimu ambayo imetolewa na daktari zinatisha kwani asilimia 59 na zaidi ya watoto chini ya miaka mitano na akina mama wajawazito vifo vyao vinatokana na changamoto hiyo,” amesema.

Ameongeza kuwa baada ya vidonge hivyo kutolewa na kusambazwa nchini anaamini itasaidia kupunguza changamoto hiyo na kuhimalisha afya wa watoto hao na muhimu kwa wazazi kuhakikisha watoto wanapatiwa matone hayo.

 Aidha, amesema Shirika la NI, limetoa vidonge milioni 500 duniani kote na Tanzania imepata vidonge milioni 22 kulingana na idadi ya watoto walipo nchini ambao ni milioni 22.

 Naye Mwakilishi wa Balozi wa Canada hapa nchini, Helen Fytche amesema mwaka 2020 kutokana na kuwepo kwa changamoto ugonjwa wa Uviko 19 watoto milioni 100 walikosa chanjo hiyo kwa awamu moja

N a kutokana na changamoto hiyo kujitokeza mwaka 2021 walifanikiwa kutoa chanjo ya vitamin A, 124 na kusaidia kuzuia vifo vya watoto milioni 32 duniani na katika kipindi hiki wamefanikiwa kuokoa vifo vya watoto milioni saba.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sixtus Mapunda, akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesema kutokana na kuelewa umuhimu wa matone hayo watahakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ili kufanikisha mchakato huo kwa asilimia kubwa.

 

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dk Godwin Mollel  amesema elimu ya mtoto inaanza siku mimba inapotunga na sio shuleni kwa kumpatia Mama lishe ili bora wakati wa ujauzito itakayosaidia kuimarisha ubongo wa mtoto.

Hivyo, ametoa wito kwa jamii hususan wazazi kuzingatia Lishe Bora kwa tangu mimba inapotungwa kwa lengo la kusaidia mtoto atakayezaliwa kuwa na afya njema hadi anapofikia hatua ya kuanza shule atakuwa na uelewa mzuri darasani.


Mwakilishi wa Balozi wa Canada hapa nchini, Helen Fytche akizungumza.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt Edwin Mollel, akizungumza katika makabidhiano hayo.


3 comments:

  1. ProperNutritionis your first defense against illness and fatigue.

    ReplyDelete
  2. Good Nutrition
    starts with mindful grocery shopping and home-cooked meals.

    ReplyDelete
  3. From macro tracking to recipe suggestions, AI reshapes Nutrition with ease.
    Healthy living has officially entered the AI era.

    ReplyDelete