RAIS SAMIA AAGIZA SEKTA YA NISHATI ISIMAMIWE VIZURI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Tuesday, March 5, 2024

RAIS SAMIA AAGIZA SEKTA YA NISHATI ISIMAMIWE VIZURI


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akizungumza mara baada ya kumuapisha  Dkt. James Peter Mataragio kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Ndogo Tunguu, Zanzibar tarehe 05 Machi, 2024.


NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema sekta ya Nishati ina uhusiano wa moja kwa moja na maendeleo ya uchumi na maisha ya kila siku ya mwanadamu.

Amesema ni lazima wanaosimamia sekta hiyo wahakikishe wanatimiza wajibu wao kwa uzalendo mkubwa na wajitahidi kuzingatia kanuni zote za utunzaji wa mitambo na miundombinu inayotoa nishati ili iwe kwenye hali nzuri wakati wote.

Ametoa maagizo hayo kwa Wizara ya Nishati, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) pamoja na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) wakati wa hafla ya uapisho wa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. James Mataragio iliyofanyika Ikuru Ndogo, Tunguu.

Aidha Rais Samia ametaka kuwepo na mwendelezo wa utoaji wa taarifa ya mara kwa mara ndani ya Serikali na kwa umma iwapo kuna matengenezo au hitilafu ili ijulikane ili kuepusha manung’uniko yanayosababishwa na kutokuwa na taarifa.

Kuhusu gesi, Rais Samia ameitaka wizara hiyo kuhakikisha inatengeneza mpango maalum wa usambazaji wa gesi ili iwe rahisi kualika sekta binafsi iweze kushirikiana nao na hivyo kufikia lengo lililokusudiwa la asilimia 85 ya kaya ziwe zinatumia nishati safi ifikapo mwaka 2031.

Pia amesema zipo nchi ambazo zimeonesha nia ya kufanya kazi na Tanzania katika masuala ya gesi, hivyo ni muhimu kuangalia sheria na miongozo inayoifunga Serikali kukaribisha sekta binafsi na kufanyia marekebisho.

 


No comments:

Post a Comment