WATUMISHI WA NISHATI WATOA ELIMU YA NISHATI SAFI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Saturday, March 9, 2024

WATUMISHI WA NISHATI WATOA ELIMU YA NISHATI SAFI





NA MWANDISHI WETU

WANAWAKE ambao ni Watumishi wa Wizara ya Nishati, wameungana na wenzao duniani kuadhimisha siku ya wanawake ambayo imeadhimishwa wilayani Chamwino mkoani Dodoma.


Katika madhimisho hayo watumishi wametumia siku hiyo kuelimisha wananchi mbalimbali kuhusu nishati safi ya kupikia.


Akitoa elimu  kwa baadhi ya wananchi Joyce Msangi afisa Misitu, alisema utumiaji wa nishati safi ya kupikia unalinda afya za walaji na inamuepusha mtumiaji na madhara mbalimbali


Aliyabainisha madhara hayo, ni pamoja na adhari kwenye mfumo wa  upumuaji na inaharibu mazingira yanayotuzunguka.


Naye, Talkisia Erio Ofisa Kumbukumbu, amewahimiza wanawake wa Dodoma kutumia nishati safi ya kupikia ili kuweza kujikwamua kiuchumi.


Kwasababu matumizi ya nishati safi ya kupikia yanauwezo wa kuhudumia watu wengine kwa muda mchache na kufanya mambo mengine ya kujikwamua kiuchumi.


Aidha, wanawake hao wamewashukuru watumishi hao na kuahidi kwenda kufanyia kazi elimu hiyo waliyoipata.


Katika Madhamisho hayo, yaliyofanyika katika viwanja vya shule   ya Chinagali Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima.

No comments:

Post a Comment