NA MWANDISHI WETU, DODOMA
MADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameaambiwa ni vema wakaithamini kazi yao na kujijali wenyewe ili kuondoa dhana iliyojengeka kuwa kundi hilo limekuwa likivunja sheria za usalama barabarani.
Akizungumza alipokuwa akitoa mafunzo ya usalama barabarani kwa madereva bodaboda Kata ya Uhuru jijini Dodoma, Polisi Kata wa Kata hiyo amesema kundi hilo la bodaboda linapaswa kutambua umuhimu wao sambamba na kuthamini kazi wanayofanya ya kutoa huduma ya kusafirisha abira.
Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika la Amend Tanzania kwa kushika na Ubalozi wa Uswisi nchini.
Amesema kumekuwapo na dhana kuwa, waendesha bodaboda wengi hawazingatii sheria za usalama barabarani, hivyo kuhatarisha maisha yao, abiria wanaowabeba na usalama wa vyombo vyao.
Kwa mujibu wa polisi Kata huyo, mafunzo wanayo yatoa ni muhimu kwa kuwa yanawawezesha bodaboda kufahamu usalama wao na jinsi ya kuvimudu vyombo wanavyoviendesha wawapo barabarani.
Kwa upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata ya Uhuru Fatma Amri anasema mafunzo hayo kwa kiasi kikubwa yanawasaidia vijana katika Kata yake kujitambua na kuzingatia sheria wanapoendesha vyombo vya moto.
Amewasisitiza bodaboda waliopata mafunzo hayo kuhakikisha waafanyia kazi elimu waliyopewa kwa kuzingatia na kuzitekeleza kikamilifu sheria za usalama barabarani.
Kupitia mafunzo hayo waendesha bodaboda hao walielimishwa kuhusu huduma ya kwanza na umuhimu wake, pia usalama wao katika maeneo yao ya kazi.
Mfunzo hayo ambayo yanatolewa kwa ufasdhili wa Ubalozi wa Uswisi yamefanyika kwa bodaboda kuingia darasani na kwa njia ya vitendo kwa lengo la kuwajengea uwezo maofisa usafishaji wote watakaohudhuria mafunzo hayo.
No comments:
Post a Comment