NA MWANDISHI WETU
KATIKA kuhakikisha usalama wa maisha ya watu wilayani Rufiji, Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imefanya msako wa mamba wanaotajwa kutishia maisha ya watu kutokana na kusogea karibu na makazi ya watu kufuatia kusafirishwa na mikondo ya maji yaliyosababishwa na mafuriko.
Ofisa habari wa TAWA Beatus Maganja akizungumza na waandishi wa habari katika mji mdogo wa utete wilayani Rufiji leo Aprili 18, 2024 amesema TAWA inaendelea na msako wa mamba tishio kwa maisha ya watu wilayani humo lengo likiwa ni kulinda usalama wa wananchi wa wilaya hiyo.
" Ni wajibu wetu kuimarisha ulinzi ili yasitokee maafa ya binadamu kupotea kutokana na kuliwa na mamba wakati sisi tuko hapa" amesema Afisa habari huyo.
"Na ndiyo maana tumekuja hapa kuhakikisha tunawasaka mamba wote ambao ni tishio kwa maisha ya binadamu.
Aidha Maganja amesisitiza kuwa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Sura ya Na. 283 inaelekeza kuwadhibiti wanyamapori wakali.
No comments:
Post a Comment