BRELA YATAJA FAIDA ZA KURASIMISHA VIWANDA - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Wednesday, June 19, 2024

BRELA YATAJA FAIDA ZA KURASIMISHA VIWANDA


NA MAGENDELA HAMISI


MKURUGENZI wa Leseni kutoka Wakala Usajili Leseni za Biashara (BRELA), Andrew Mkapa amesema  miongoni mwa faida kadhaa za kusajili Viwanda ni pamoja na kupata fursa za vivutio vinavyotolewa na Serikali katika nyakati tofauti ikiwemo mafunzo au tofauti na hiyo.


Licha ya kupata fursa ambazo Serikali inatoa kwa nyakati fulani, amesema pia mwekezaji anaposajili anakuwa ametii sheria bila shuruti inayosaidia kupunguza mivutano isiyokuwa ya msingi baina ya pande hizo mbili.


Hayo amebainisha leo, Juni 19, 2024  mkoani Morogoro wakati akiwasilisha mada inayohusu Leseni za Viwanda kwa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Dar es Salaam wanaoudhuria mafunzo  yenye lengo la kuwaongezea uelewa namna ya kuripoti taarifa na shughuli zinazotolewa na Brela bila kupotosha umma.


"Pia mwekezaji anaposajili/ kurasimisha kiwanda, Serikali inapata takwimu sahihi ya viwanda vilivyopo nchini na aina ya bidhaa ambazo inazalishwa ili kuweka mipango stahiki kwa maendeleo yao na mapato ya Serikali kuongezeka yanayotokana na ada ambayo ni sawa na gharama za kuendesha  huduma hiyo" amesema.


Pia ameongeza kwa mujibu wa sheria iliyopo, ada kwa viwanda vikubwa na kati wanatakiwa kulipa shilingi 800,000 kwa uwekezaji unaozidi milioni 100 na kupatiwa leseni.


Mkapa ameongeza kuwa uwekezaji wa Sh.milioni 5 atalipiwa Sh. 10,000, unaozidi mil 5, analipiwa sh.50,000 na unaozidi mil 10, atalipia sh.100,000 na wote watalipa ada mara moja tu na kupewa leseni  ya kudumu  kwa uwekezaji wa viwanda vikubwa na kati, viwanda vidogo wanapewa cheti cha usajili.


Pia ameongeza kuwa kutokana na kuwa na mfumo madhubuti ambao Brela imeutengeneza unaoitwa ORS ,  mwekezaji anaweza kufanya usajili popote halipo na kwa urahisi unaonzia kupitia mfumo wa Serikali unaoitwa the TNBP ( www.business.og.tz ).

Ameongeza kuwa maombi yote ya usajili yanachukua kuanzia saa moja hadi siku tatu kulingana na changamoto zitakazojitokeza wakati mchakato wa usajili.

Amebainisha kuwa moja ya changamoto ambazo wanakutana nazo katika kukamilisha michakato ya usajili ni pamoja mtandao unapokuwa chini kwa baadhi ya taasisi.







No comments:

Post a Comment