NA MWANDISHI WETU, KAGERA
MAHAKAMA ya Wilaya ya Bukoba imemhukumu, Sadati Rweyemamu ambaye ni Wakala na mfayabiashara wa kuuza pikipiki Kagera kwa kosa la ukwepaji kodi kwa kutotoa EFD receipt na kupelekea kukwepa kodi ya kiasi cha Sh.5,949,152.
Adhabu hivyo imetokana na mshtakiwa kushtakiwa kwa Rushwa kinyume na kifungu cga 15 (1) (a), 2 cha PCCA na Kujipatia fedha na manufaa yasiyostahili baada ya kuuza pikipiki kumi zenye thamani ya sh. 39,000,000/- na Kosa la Kutotumia Risiti ya Efd katika mauzo hayo kinyume na kif. cha 86 (1), (b) na (3) cha Sheria za Usimamizi wa Kodi Sura ya 438 Marejeo ya 2022.
Hukumu hiyo dhidi ya Rweyemamu katika kesi ya rushwa namba 15406/2024 imesomwa na Andrew Kabuka, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Bukoba, mbele ya Wakili wa Jamhuri (PCCB) Kelvin Murusuri.
Mshitakiwa ametiwa hatiani kwa kuamriwa kulipa faini ya sh 3,000,000 au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela. Pia Mahakama kutokana na maombi ya Wakili Murusuri imemuamuru mshtakiwa kulipa kodi hiyo ya Serikali sh. 5,949,152/- ndani ya miezi mitatu.
Mshtakiwa amekwenda Gerezani kungojea taratibu za upatikanaji wa fedha za kulipia faini.
No comments:
Post a Comment