TUONDOKANE NA MATUMIZI YA NISHATI ISIYO SAFI KULINDA AFYA ZETU - MWANAIDI - MAGENDELA BLOG

Breaking

Recent-Post

ads header

Friday, October 18, 2024

TUONDOKANE NA MATUMIZI YA NISHATI ISIYO SAFI KULINDA AFYA ZETU - MWANAIDI


NA MWANDISHI WETU

NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia,  Wanawake na Makundi Maalum,  Mwanaidi Khamis ametoa rai kwa jamii kuondokana na matumizi ya nishati zisizo safi ili kulinda afya zao.


Ameyasema hayo jijiini Dodoma  wakati akihamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati isiyo safi na kuanza kupika kisasa kwa kutumia nishati iliyo safi.


"Jamii ihamie katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kulinda afya na magonjwa,  lakini pia majiko haya ya kisasa tunayopikia ni salama.' Amesema Khamis


Amesema wanawake  ndio wamekuwa wahanga wakubwa wa athari zitokanazo na matumizi ya nishati zisizo safi ikiwemo magonjwa ya mapafu. 


Ameongeza kuwa, mbali ya athari kwa binadamu,  matumizi ya nishati isiyo safi pia husababisha uharibifu wa mazingira kutokana na ukataji wa kuni na mkaa.


Ametanabaisha kuwa,  uharibifu wa mazingira unasababisha mabadiliko ya tabianchi ikiwemo upatikana wa mvua zisizo tabirika pamoja na kuathiri vyanzo vya maji ambayo pia yanatumika katika uzalishaji wa nishati ya umeme.

No comments:

Post a Comment