NA DOTTO MWAIBALE
SERIKALI imeshakusanya
jumla ya Sh.Bilioni 325.3 katika kipindi cha miezi mitano (Aprili hadi Septemba
2024) tangu DPW Dar es Salaam waanze kuendesha Gati 0-7 katika Bandari ya Dar
es Salaam.
Hayo
yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na
Msemaji wa Serikali, Greyson Msigwa wakati akitoa taarifa kuhusu masuala
mbalimbali yaliyotekelezwa na Serikali katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika Desemba 19, 2024 jijini Dar es Salaam.
“ Mapato
haya yanayotokana na shughuli za mikataba iliyoingiwa kati ya TPA na DP World,
ikijumuisha tozo ya pango (land rent), tozo ya mrahaba (royalty), na Ardhia (warfage),
alisema Msigwa.
Msigwa
alisema kutokana na kuongezeka kwa mapato na kupungua kwa gharama za uendeshaji
kufuatia maboresho yaliyofanyika, Serikali, kupitia TPA, imeanza uwekezaji
katika miradi yenye thamani ya TZS 1.922 trilioni (USD 686.628 milioni) kwa
kutumia makusanyanyo yanayopatikana.
Alisema
miradi hiyo ni Ujenzi wa Kituo cha Kupakulia Mafuta (SRT); Ujenzi wa Bandari ya
Kisiwa Mgao (Mtwara) na Ujenzi wa Gati za Majahazi (Dhow Wharf) Dar es Salaam.
Msigwa
alisema kuunganishwa kwa mifumo ya forodha (Tanzania Customs Integrated System
- TANCIS) na ile ya bandari (Tanzania Electronic Single Window System-TeSWS)
imewezesha kupunguzwa na kuondolewa kwa mifumo iliyokuwa inafanana na hivyo
kupunguza muda wa kuondoa mizigo bandarini, kuongeza uwazi na kurahisisha
mawasiliano.
Alisema mapato ya kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yameongezeka hadi kufikia TZS Trilioni 1 mwezi Septemba 2024 ikilinganishwa na wastani wa TZS 850 Bilioni kwa mwezi na kuwa hali hiyo metokana na TRA kuweza kuchakata mizigo mingi zaidi ndani ya muda mfupi.
“Kwa ujumla wake, maboresho yanayoendelea katika Bandari ya Dar es Salaam kufuatia kukabidhiwa kwa DP World na makampuni mengine kuendesha Bandari ya Dar es Salaam yanaonesha kuwa na faida kubwa kiuchumi kwa kuchochea kuongezeka kwa biashara na kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini na ni sehemu muhimu ya utekelezaji wa azima ya serikali ya kuifanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa lango kuu la usafirishaji mizigo katika ukanda wa Afrika,” alisema Msigwa.
Msigwa
akizungumzia uwekezaji katika Bandari ya Tanga alisema Serikali imefanya
uwekezaji mkubwa wa zaidi ya Sh. Bilioni 429 kwa awamu mbili kuboresha bandari hiyo
hatua ambayo imeongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali kutokana na wingi wa
shehena inayopita katika bandari hiyo.
Alisema katika
kipindi cha miezi 3 ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha 2024/25 bandari ya
Tanga imevuka lengo kwa kukusanya mapato kiasi cha Sh.Bilioni 18.6 ambayo ni
zaidi ya lengo lililowekwa la kukusanya Sh. Bilioni 11 na kuwa mapato hayo ni
zaidi ya mapato yote yaliyokusanywa katika mwaka wa fedha 2019/2020 ya kiasi
cha Sh.Bilioni 16.
Aidha, Msigwa alisema meli zenye ukubwa tofauti zimekua zikitia nanga katika bandari hiyo hatua inayoongeza kiwango cha bidhaa na shehena ambazo awali zilikua hazipiti katika bandari hiyo zikiwemo shaba (copper) tani 33,000, Ammonium nitrate tani 41,000 na Sulphur tani 100,004.
Msigwa
alisema Serikali imeendelea kuimarisha miundombinu ya Bandari za Dar es Salaam,
Mtwara,Tanga na zile zilizopo kwenye maziwa hali iliyochangia kuongeza ufanisi
katika kuhudumia shehena ambapo katika kipindi cha mwezi Mei 2024 hadi Novemba
2024, kiwango cha shehena kilichohudumiwa na bandari zote zilizo chini ya
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ni tani milioni 16.5 ambayo ni
zaidi kwa asilimia 5.92 ya shehena milioni 15.6 iliyohudumiwa katika kipindi
kama hiki kwa mwaka uliopita (Mei 2023 hadi Novemba 2023)
Alisema kwa upande wa idadi ya Makasha yaliyohudumiwa na bandari zote zilizo chini ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania katika kipindi cha Mei 2024 hadi Novemba 2024 ilifikia makasha 621,584 sawa na ongezeko la asimilia 3.29 ya makasha 601,805 yaliyohudumiwa katika mwaka uliopita (Mei 2023 hadi Novemba 2023).
Katibu huyo
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Mchezo, Greyson Msigwa
akizungumzia utendaji kazi wa Bandari ya Dar es Salaam katika kipindi cha mwezi
Mei, 2024 hadi Novemba 2024, kiwango cha shehena kilichohudumiwa na Bandari ya
Dar es Salaam ni tani milioni 14.4 ambayo ni zaidi ya asilimia 5.6 ya shehena
milioni 13.7 iliyohudumiwa katika kipindi kama hiki mwaka uliopita (Mei 2023
hadi Novemba 2023).
Alisema shehena
ya Makasha (Containers-TEUs) Idadi ya Makasha yaliyohudumiwa na Bandari ya Dar
es Salaam katika kipindi cha Mei 2024 hadi Novemba 2024 ilifikia makasha (TEUs)
598,672 sawa na ongezeko la asimilia 0.2 ya makasha (TEUs) 597,613 yaliyohudumiwa
katika kipindi kama hicho mwaka uliopita (Mei 2023 hadi Novemba 2023).
Alisema
bandari hiyo Shehena ya Nchi jirani katika kipindi cha Mei, 2024 hadi Novemba
2024 ilihudumia shehena tani milioni 6.3 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia
19.3 ya shehena ya nchi jirani iliyohudumiwa katika kipindi kama hicho mwaka
uliopita (Mei 2023 hadi Novemba 2023) ambayo ilikua tani milioni 5.3. ambayo
ilikuwa kubwa kuliko ya kipindi kama hicho
mwaka 2023.
Msigwa
alitaja baadhi ya mafanikio baa ya uwekezaji wa DP World kuwa Serikali kupitia
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ilisaini mikataba mitatu ya
uwekezaji na kampuni ya DP World (Dubai) tarehe 22 Oktoba, 2023. Mkataba huo
ulihusisha uendeshaji wa shughuli za bandari katika uhudumiaji wa makasha,
mizigo mchanganyiko na shehena ya magari.
Alisema ili kutoa huduma hizo kwa kuzingatia sheria za nchi yetu, Kampuni ya DP World ilifungua kampuni ya Tanzania inayoitwa DP World Dar es Salaam iliyokabidhiwa rasmi shughuli za uendeshaji wa bandari Aprili 15, 2024 na kuwa tangu kampuni hiyo ianze uendeshaji wa shughuli za bandari mafanikio mbalimbali yamepatikana.
Alitaja mafanikio mengine kuwa kwa mujibu wa mkataba, Kampuni ya DPW ilipaswa kuwekeza Dola za Kimarekani milioni 250 (TZS bilioni 675) katika kipindi cha miaka mitano lakini katika kipindi cha miezi mitano tayari wameshawekeza TZS 214.425 bilioni (31%) kwa ajili ya manunuzi ya mitambo ya kisasa, ukarabati wa mitambo iliyokuwa ya TPA na usanifu na usimikaji wa mfumo wa TEHAMA wa kisasa wa uendeshaji wa Bandari.
No comments:
Post a Comment