AMANI Masisi, mkazi wa jijini Mbeya amefanikiwa kufunga mwaka 2024 kwa kutwaa zawadi ya Pikipiki, katika droo ya pili ya promosheni ya Santa Mizawadi inayoendeshwa na kampuni ya mtandao wa simu ya mkononi ya Airtel.
Meneja Mawasiliano wa kampuni hiyo, Jenipher Mbuya, amesema lengo la promosheni hiyo ni kurejesha shukrani kwa wateja wao kwa kutumia huduma za kampuni hiyo na kuifanya kuendelea kufanya vema hapa nchini.
"Wenyewe mmeona namna droo inavyoendeshwa kwa uwazi tukiwa chini ya usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha na hakika inaendeleza furaha kwa wateja wetu, na wale ambao bado hawajajiunga na mtandao wetu, wajiunge ili waweze kunufaika na zawadi zetu katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka," amesema.
Ameongeza kuwa namna ya kushiriki katika promosheni hiyo na kujishindia Santa Mizawadi, kwa upande wa Wakala wa Airtel anatakiwa kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha.
Pia kwa mteja anachotakiwa kufanya ni kununua bando, kulipa bili, kutuma na kutoa fedha, kununua muda wa maongezia au vifurushi kupitia *149*99#, *150*60# au kupitia 'My Airtel App'.
Katika droo hiyo ambayo imechezeshwa leo, Desemba 31, 2024 Batuli Shichambo wa jijni Tanga, ametwaa zawadi ya Router yenye uwezo wa 5G, pia Ngusa Konzongwe mkazi wa Kariua mkoani Tabora na Mangi Ibrahim wamejishindia simu ya mkononi aina ya smartphone.
Naye, Seigule Mollel mkazi wa Longido jijini Arusha amejishindia runinga Inchi 55 na Jumanne Kigomba ambaye ni mkulima mkazi wa Kibiti mkoani Pwani amejishindia shilingi ml. 1
Baada kutamatika kwa droo hiyo ya awamu ya pili ya promosheni ya Santa Mizawadi inayofanyika kila Jumanne kwa kipindi cha mwezi mmoja, Jenipher amesema kuwa, washindi wote watafikishiwa zawadi popote walipo baada ya taratibu kukamilika.
No comments:
Post a Comment