NA MWANDISHI WETU
WAKATI joto la Uchaguzi Mkuu
utakaofanyika nchini kote Oktoba mwaka huu likizidi kupanda wafanyabiashara jijini
Dar es Salaam kutoka nje ya nchi wametakiwa kutokuwa na hofu kwani ulinzi na
usalama wa mali zao umehimarishwa.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dar
es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila alipozungumza na
waandishi wa habari na hakusita kupongeza mafanikio yanaendelea kupatikana
kupitia maboresho ambayo yamefanywa na Mamlaka ya Bandari.
Amefafanua kuwa wanasiasa wengi wanakiri kuwa Serikali imefanya makubwa katika ujenzi wa miradi mbalimbali kupitia makusanyo ya ndani, hivyo kinachotakiwa sasa ni wananchi kuendelea kulipa kodi ili miradi mingine ya kimkakati ifanyiwe kazi ipasavyo.
"Kwa sasa tupo katika kipindi
kinacholekea kwenye Uchaguzi Mkuu, hivyo inawezekana baadhi ya wafanyabiashara
wakawa na hofu, ninachoweza kuwaambia wasiwe na hofu kwani Mkoa umejipanga kuhakikisha
utulivu na amani inaendelea kutawala kabla na baada uchaguzi, "amesema.
Ameweka wazi kwamba hakuna taasisi,
chama cha siasa, mashirika mbalimbali yatakayoweza kuvuruga amani iliyolindwa
tangu zamani kutokana na misingi imara ya kiungozi hususan wa Rais Dkt Samia
Suluhu Hassan.
Ameongeza kuwa inawezekana
ipo taasisi au makundi mengine yanaweza kuwa na malalamiko, hivyo kinachotakiwa
ni kutumia haki zao za kimsingi vizuri kwa kufuata sheria nchi ili kuendelea
kuifanya Dar es Salaam na Tanzania kwa ujumla kuwa na amani wakati wote.
Aidha amebainisha kuwa uongozi wa
mkoa unafanya jitihada kadhaa ili kila mmoja asiwe na malalamiko katika kipindi
hiki kinachoelekea kufanyika kwa uchaguzi mkuu na lengo ni moja tu, Dar es
Salaam na Tanzania iendelee kudumu
katika misingi ya amani na utulivu.
“Kwa sasa kama Mkoa tunasubiri taarifa ya Tume
Huru ya Uchaguzi ili kupata taarifa kamili waliojitiandikisha na kusahihisha
taarifa ili tuwezo kutoa ushirikiano wa kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa
amani na utulivu, niwaombe wafanyabishara wandelee na shughuli zao kama kawaida
saa 24,” amesema.
Amefafanua kuwa baada ya kuzindua
biashara kufanyika saa 24 hali inaendelea vizuri na mchakato ambao kwa sasa upo
ni kwa wakuu wa Wilaya nao kujipanga katika maeneo yao ili wazindue biashara
kufanyika saa 24 kama ambavyo mkoa imefanya.
Akizungumzia kuhusu Soko Kuu la
Kariakoo, amebainisha kuwa limekamilika kwa asilimia 95 na wafanyabishara zaidi
ya 1500 wameidhinisha na mchakato ambao unaendelea ni kuingia nao mikata
kufanya shughuli zao hapo.
Pia amesisitiza mchakato mwingine ambao unaendelea ni kupitia madeni yote ya wafanyabishara ya nyuma kuhakikisha wanalipa kabla ya mchakato mwingine kuendelea.
“Naomba wakati michakato kadhaa
ikiendelea viongozi wa wafanyabiashara kuhakikisha wanafungua njia ambazo
zimezibwa na wafanyabishara wadogo bila shuruti ili kutoa nafasi kwa viongozi
kupita kukagua asilimia zilizobaki hususan uzio ambao unaendelea kujengwa,” amesema
Akizungumzia mafanikio ambayo
yamepatikana katika kipindi cha miaka minne, amesema anayojivua kwa sasa na kuwepo
fungu kwaajili ya ujenzi ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itakayojengwa kisasa kulingana
na mahitaji yaliyopo.
Kuhusu ujenzi wa Daraja la
Jangwani, amesema tayari mhandisi wa ujenzi ameshaanza kazi na anachofanya ni
kujenga kambi za kuweka vifaa na ni dhahiri changamoto iliyokuwepo kwa kipindi
kirefi inakwenda kuondoka, pindi daraja litakapokamilika.
Chalamila pia ameongeza kuwa wananchi ambao
waliondolewa eneo la kipawa, mchakato unaendelea wa kuhakikisha wananchi hao
wanendelea kulipwa hatua kwa hatua na hakuna ambaye hatolipwa.
No comments:
Post a Comment