DKT. YONAZI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA TFNC - MAGENDELA BLOG

Recent-Post

ads header

Tuesday, April 15, 2025

DKT. YONAZI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA TFNC


NA MWANDISHI WETU - DODOMA


KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania Dkt. Germana Leyna kwa lengo la kujadili maandalizi ya kuelekea Mkutano Mkuu wa Wadau wa Lishe kwa mwaka 2025 ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Agosti, 2025.


Kikao hicho kimefanyika katika ofisi yake Jijini Dodoma, ambapo Katibu Mkuu ameusii uongozi wa Taasisi hiyo kushirikiana na Ofisi yake kuandaa mkutano wenye viwango ili uendelee kuleta tija kwa Taifa na mafanikio makubwa kama inavyokusudiwa.


Kikao hicho kimeudhuriwa na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu wakiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa Shughuli za Serikali, Paul Sangawe, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Ofisi hiyo, Augustino Tendwa, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA Einhard Mbuge, Mratibu wa Masuala ya Lishe Ofisi ya Waziri Mkuu Abigael Marwa,  Fredrick Maduma Mchumi Ofisi ya Waziri Mkuu,  Spora Mwakinga Mchumi, pamoja na watendaji kutoka Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania akiwemo Afisa Habari wa Taasisi hiyo, Jackson Monela.





No comments:

Post a Comment