NA MWANDISHI WETU
RAIS DKT. Samia Suluhu Hassan ametajwa kuwa ni msikivu pindi anapopelekewa changamoto kuzitatua.
Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Mawasiliano na teknolojia, Jerry Silaa wakati wa Tamasha la Mtoko wa Pasaka ambalo limeandaliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Ongea na Mwanao inayoongozwa na Steven Mengele Steve Nyerere'.
Amesisitiza kuwa baadhi ya wanasiasa pindi wanapopata nafasi ya kuzungumza na waandishi watumie vizuri ili wasiharibu amani ya nchi maana ikitoweka inakuwa ngumu kuirejesha.
Amesistiza kuwa amani ni tunu ya Taifa inatakiwa kulindwa Kwa njia ya yoyote ikiwemo ya mazungumzo hivyo wanapokuwa na changamoto Rais ni msikivu anawasiliza, amesema.
"Kaulimbiu ya Tamasha hili 'Kwa maombi utashinda'ni kielelezo cha jitihada za kuendelea kuitunza amani tuliyonayo.
"Ukiangalia hata huko mitandaoni utaona adha ambayo wanaipata wananchi ambao nchi zao zina machafuko na hakika utaona kuwa amani tuliyonayo si ya kuichezea" amesema Silaa.
No comments:
Post a Comment